DC NYAKIA MGENI RASMI UFUNGUZI WA UPIMAJI AFYA POLISI RUKWA


Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Mhe. Nyakia Ally Chilukile, amekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa huduma ya upimaji wa afya kwa magonjwa yasiyoambukizwa, zoezi lililoandaliwa na Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Afya cha Polisi nchini. Uzinduzi huo kwa mkoa wa Rukwa umefanyika Julai 5, 2025, katika viwanja vya Polisi Wilaya ya Sumbawanga, ukiambatana na mazoezi ya mbio za pole pole (jogging) yaliyoshirikisha vyombo vya ulinzi na usalama, vilabu vya michezo na wananchi wa kada mbalimbali.


Katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Ummy Nderiananga, alihudhuria na kusisitiza umuhimu wa utunzaji wa afya kwa maendeleo ya taifa, akieleza kuwa afya bora ni msingi wa taifa imara. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, SACP Shadrack Masija, naye alitumia fursa hiyo kuhimiza mazoezi ya mwili kama njia ya kuimarisha afya, kuongeza tija kiuchumi na kuboresha mahusiano ya kifamilia.


Huduma hiyo ya upimaji wa afya imelenga kuhamasisha jamii na watumishi wa vyombo vya usalama kujijengea utaratibu wa kufuatilia afya zao mara kwa mara ili kuepuka athari za magonjwa yasiyoambukizwa.


@sumbawanga_municipalcouncil



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

DUNIA NI KATILI SANA KWA MWANAUME MASIKINI

MAKUNDI YA VILABU VINAVYOSHIRIKI KOMBE LA DUNIA 2025.

JINSI YA KUMTAWALA MWANAMKE HASA MKE (USIOE MKE WA MTU)

MUONEKANO WA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA MSALATO

DIARRA KIPA BORA TANZANIA

CHINYELE ACHUKUA FOMU KUOMBA RIDHAA YA KUGOMBEA UBUNGE DODOMA MJINI