MAMBO 7 MUHIMU YA KUYAEPUKA BAADA YA KUACHANA...


i. Kutafuta Mtu Mbadala Kwa Haraka Kabla Moyo Haujapona


ii. Kufanya Mambo Ili Umuoneshe Kuwa Unaendelea Vizuri


iii. Kuchukia Kila Mtu Hata Wasiohusika


iv. Kufanya Mbinu Za Kumdhuru


v. Kuhitimisha Hautapata Mtu Mwingine 

Kama Yeye


vi. Kujingiza Kwenye Tabia Hatarishi Ili Kupoteza Mawazo


vii. Kujiondolea Thamani


Katika Makala Hii Tutazungumzia Jambo La Saba


- Kujiondolea Thamani


Kuachana na mtu kunaweza kukuondolea kabisa thamani yako unayojipa. 


Yaani unaweza kujiona kuwa hauna thamani tena na hakuna anaekutaka tena. 


Usisahau kuwa, unaweza kuachana na mtu na tatizo lisiwe kwako bali likawa kwake.


Sio kila wakati unapoachana na mtu basi ni wewe haufai, inawezekana ni yeye ndiye hakufai. 


Usijihukumu na kujiondolea thamani. 


Wewe bado ni wa thamani na kuna wengi wanakuhitaji. 


Yaani, wewe ni ndoto ya watu fulani, wanatamani kukupata. 


Ndio ile msemo wa kiswahili wanasema...


“Wakati mwingine anasema ni wa nini, kuna mwingine anajiuliza nitampata lini?”


Thamani yako haiondoki kwa sababu umeachana na mtu.


Thamani yako inaondoka utakapoanza kujidharau. 


Usisahau kuwa, ukitupa dhahabu kwenye zizi la ng’ombe wataikanyaga. 


Inawezekana pia wewe ni dhahabu iliyokuwa imewekwa mahali pasipo sahihi. 


Usijikatae, wala usijidharau wewe bado ni wa thamani. 


“Don’t let someone who isn’t worth your love make you forget how much you are worth.” — Elizabeth Karls


Kama umependa makala hii tafadhali share na wengine.


See You At The Top


Dr. Joel Arthur Nanauka

 


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WALIOKUWA WABUNGE WALIOPITIWA NA MKASI WA WAJUMBE

MWANAUME USIPITWE NA HILI, INASIKITISHA...?!!!

USAJILI ULIVYO HADI SASA....

HUYU NDIYE MWANAMKE WA KUOA

SPIKA MSTAAFU NDUGAI AFARIKI DUNIA

RAIS SAMIA AYATAKA MASHINDANO YA MISS WORLD 2027

MWENYE MASIKIO NA ASIKIE....