SIFURAHII YANGA IKIIFUNGA SIMBA - HERSI

Rais wa Klabu ya Yanga SC na Mwenyekiti wa Vilabu Barani Afrika, Eng. Hersi Said, amesema kuwa hana furaha yoyote binafsi pale timu yake inapowashinda watani wao wa jadi, Simba SC, akibainisha kuwa anafanya hivyo kwa kuwa anatekeleza wajibu wake wa kuiongoza Yanga kupata matokeo mazuri.


"Kama kuna jambo silipendi, ni kutoa furaha za watu. Najua kuna ndugu zangu ambao ni Simba na mimi ni Yanga," alisema Eng. Hersi.
"Bahati mbaya taasisi ambayo naishughulikia ni taasisi inayotaka matokeo, na kwa sababu ya 'nature' ya taasisi, unalazimika kutafuta matokeo."

Hersi aliongeza kuwa kwa nafasi yake kama kiongozi wa klabu kubwa kama Yanga SC, anapaswa kuweka maslahi ya timu mbele na kuhakikisha inapata ushindi, bila kujali hisia za ushindani wa jadi uliopo.


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

DUNIA NI KATILI SANA KWA MWANAUME MASIKINI

MWANAUME USIPITWE NA HILI, INASIKITISHA...?!!!

USAJILI ULIVYO HADI SASA....

HUYU NDIYE MWANAMKE WA KUOA

RAIS SAMIA AYATAKA MASHINDANO YA MISS WORLD 2027

MAMBO 7 MUHIMU YA KUYAEPUKA BAADA YA KUACHANA...