RAIS WA BURKINA FASO ATANGAZA DIRA YA KUUNDA MUUNGANO WA MATAIFA YA AFRIKA (UNITED STATES OF AFRICA).

Katika hatua ya kihistoria inayolenga kuunganisha bara la Afrika, Rais wa Burkina Faso, Ibrahim Traorรฉ, ametangaza mpango wa kuunda "Muungano wa Mataifa ya Afrika" (United States of Africa). Mpango huu unalenga kuunganisha Nchi zote za Afrika chini ya mfumo mmoja wa kisiasa na kiuchumi. Katika mpango wake, Rais Traorรฉ anapendekeza:


- Kuanzishwa kwa Serikali moja ya bara zima.
- Utumiaji wa sarafu moja itakayojulikana kama "Afro Money".
- Kutolewa kwa pasipoti moja ya Kiafrika itakayowezesha Waafrika kusafiri bila visa ndani ya bara.
- Usambazaji wa rasilimali na utajiri wa Afrika kwa usawa kati ya Nchi zote, kuhakikisha hakuna Taifa linalobaki nyuma.

Rais Traorรฉ anaamini kuwa hatua hizi zitaimarisha mshikamano, kukuza uchumi, na kuondoa mipaka ya kikoloni iliyosababisha mgawanyiko na migogoro barani Afrika.

Mnamo Julai 6, 2024, Burkina Faso, Mali, na Niger zilitangaza kuundwa kwa Muungano wa Mataifa ya Sahel (Alliance of Sahel States - AES), ambao ni hatua ya awali kuelekea umoja wa bara zima. Muungano huu unalenga:

- Kujenga miundombinu ya pamoja ya nishati na mawasiliano.
- Kuanzisha soko la pamoja na umoja wa kifedha chini ya sarafu mpya.
- Kurahisisha usafiri kwa kutoa pasipoti ya pamoja ya AES.
- Kuwekeza katika sekta za kilimo, madini, na nishati.

Rais Traorรฉ tayari amepokea pasipoti yake ya AES, ikiwa ni ishara ya kuanza kwa hatua hii mpya ya ushirikiano wa kikanda.

Ingawa mpango huu umeungwa mkono na Vijana wengi barani Afrika wanaotamani mshikamano na maendeleo, baadhi ya Viongozi wa Afrika wameonyesha wasiwasi kuhusu kupoteza mamlaka ya kitaifa na uhuru wa kisiasa. Hata hivyo, Rais Traorรฉ anaendelea kusisitiza umuhimu wa umoja wa Afrika kama njia ya kujitegemea na kuondokana na athari za ukoloni.

Mpango huu wa "Muungano wa Mataifa ya Afrika" unaashiria mwanzo mpya kwa bara la Afrika, likiwa na matumaini ya kuleta mshikamano, maendeleo, na heshima k

#BurkinaFaso #Burkina #africa 

TOA MAONI YAKO KWENYE COMMENT 


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

DUNIA NI KATILI SANA KWA MWANAUME MASIKINI

MWANAUME USIPITWE NA HILI, INASIKITISHA...?!!!

HUYU NDIYE MWANAMKE WA KUOA

USAJILI ULIVYO HADI SASA....

RAIS SAMIA AYATAKA MASHINDANO YA MISS WORLD 2027

DIARRA KIPA BORA TANZANIA