HATIMAYE MO DEWJI AJITOKEZA

Wapenzi wa Simba,

Najua mioyo yenu imebeba maswali mengi. Kama Rais wenu, msione nimekaa kimya wakati tumepitia kipindi hiki kigumu. Kupambania Simba ni wajibu wangu.

Huu siyo wakati wa lawama ni wakati wa kusimama imara, kuwa kitu kimoja, na kuchukua hatua sahihi za kuleta mabadiliko chanya.

Katika siku chache zijazo, nitazungumza na nyie moja kwa moja. Kuna kazi kubwa inaendelea, na kuna matumaini ya kweli.

Simba haijapotea. Tumekuwa kwenye kipindi cha mpito, tumejenga kikosi kipya, tumeimarisha benchi la ufundi, na tumeweka msingi wa mwelekeo mpya. Msimu huu tumefika mbali zaidi ya matarajio, na msimu ujao tunarudi kwa nguvu mpya.

Naomba tuendelee kuwa wavumilivu. Tunahitaji kufanya marekebisho makubwa. Tuendelee kusimama pamoja kama familia moja.

Mbele yetu kuna mwanga. Na kwa pamoja, tutarudi tukiwa imara zaidi, wenye njaa zaidi, na wa kishujaa zaidi.




 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

DUNIA NI KATILI SANA KWA MWANAUME MASIKINI

MAKUNDI YA VILABU VINAVYOSHIRIKI KOMBE LA DUNIA 2025.

JINSI YA KUMTAWALA MWANAMKE HASA MKE (USIOE MKE WA MTU)

MUONEKANO WA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA MSALATO

DIARRA KIPA BORA TANZANIA

CHINYELE ACHUKUA FOMU KUOMBA RIDHAA YA KUGOMBEA UBUNGE DODOMA MJINI