Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania (UWT), Ndg. Mary Chatanda amewataka viongozi wa UWT, wabunge na madiwani wa viti maalumu walioshinda kura za maoni kuvunja makundi ili kujenga umoja utakaohakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025.
Ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza katika kikao cha ndani cha kupanga mikakati ya ushindi kilichofanyika katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam leo Agosti 29, 2025.
Amesema kuwa kwa namna moja ama nyingine katika harakati za kutafuta kura za maoni kuna baadhi ya wagombea walioshindwa watakuwa wamejeruhiwa, hivyo inatakiwa kwenda kuzungumza nao kurejesha mioyo na imani zao kwa lengo la kuumpatia ushindi mkubwa mgombea wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani.
Kikao hicho kilihudhuriwa na walioshinda kura za maoni kugombea ubunge wa Viti Maalumu kupitia mikoa, vijana na makundi maalumu. Kimehudhuriwa pia na Spika wa Bunge ambaye ni mgombea ubunge Jimbo la Uyole, Dkt. Tulia Ackson.
Kampeni zimeanza jana Agosti 28, 2025 kwa CCM kufanya uzinduzi uliofana kwenye viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe Jijini Dar es Salaam.Zitahitimishwa Oktoba 28, 2025.
Chatanda akiaga baada ya kuhitimisha kikao hicho.
Chatanda akisisitiza jambo.
Katibu Mkuu wa UWT, Suzan Kunambi akielezea baadhi ya mikakati hiyo.
Spika wa Bunge, Tulia Ackson akiaga baada ya kikao kumalizika.
baadhi ya wabunge wateule wakiwa katika kikao hicho.IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
0754264203
Comments