MKENDA - MICHEZO NI DARAJA LA AMANI NA UMOJA


NA OWM-TAMISEMI,MOROGORO


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema michezo ni nyenzo muhimu ya kujenga amani, umoja na mshikamano, kwa kuwa huwaunganisha watu bila kujali tofauti za kisiasa, kiutamaduni au mipaka ya nchi.


Prof. Mkenda ameyasema hayo leo, Agosti 16, 2026, wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Michezo ya Wanafunzi wa Shule za Afrika Mashariki (FEASSA Games 2026) kwa niaba ya Waziri Mkuu Dkt.Mwigulu  Nchemba yanayofanyika mkoani Morogoro.


Amesema FEASSA si mashindano ya kutafuta medali pekee, bali ni jukwaa la kukuza vipaji, kujenga urafiki na kuimarisha umoja wa vijana wa Afrika Mashariki.


Amesisitiza kuwa kupitia michezo, wanafunzi hujifunza nidhamu, heshima, ushirikiano na uvumilivu, mambo ambayo ni msingi wa kujenga kizazi chenye uwezo wa kuleta maendeleo katika nchi zao na Afrika Mashariki kwa ujumla.


“Michezo inatufanya tushindane uwanjani, lakini tubaki kuwa marafiki nje ya uwanja,” amesema Prof. Mkenda.


Ameeleza kuwa Serikali itaendelea kuwekeza katika michezo shuleni ili kutambua na kukuza vipaji vya vijana, huku akiwataka washiriki kutumia mashindano hayo kujifunza, kujenga urafiki na kushindana kwa nidhamu.







Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Soma Taarifa ya UTEUZI:Rais Jakaya Kikwete amemteua Dkt. Ben E. Moshi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya PUMA Energy (zamani ilijulikana kama BP Ltd)

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

OWM–TAMISEMI YASHINDA TUZO YA MABADILIKO YA KIDIJITALI KATIKA TEHAMA AWARDS 2026

KOCHA WA MC ALGERS AIHOFIA YANGA

VIONGOZI NA WATENDAJI WA MATAWI UVCCM PANGANI WANOLEWA

MAMBO 16 USIYOYAJUA KUHUSU RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA KIKWETE

NMB YAWAUNGANISHA WANANCHI NA HUDUMA, FURSA ZANZIBAR

HIZI HAPA TAKWIMU ZA PETER SHALULILE MCHEZAJI MPYA WA YANGA SC 🔰 🔥