CHENGE JELA MIAKA MITATU

Mzee wa Vijisenti leo amehukumiwa ama kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini sh 700,000 katika kesi yake ya kuendesha gari lisilokuwa na bima, bila tahadhari, na kusababisha vifo vya watu wawili. Hata hivyo alilipa faini na kuachiwa huru.

Mbunge wa Bariadi Mashariki Mh. Andrew Chenge ambaye amewahi kushika nafasi mbalimbali za juu katika serikali ya Tanzania ikiwamo ya Mwanasheria Mkuu wa serikali, leo alipona kutupwa jela miaka mitatu baada ya kulipa faini ya sh 700,000 katika kesi yake kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha vifo vya wanawake wawili.

Hakimu Mfawidhi Kwey Rusema wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ametoa hukumu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi na vielelezo vilivyoletwa mahakamani hapo.

Rusema alisema kutokana na ushahidi wa watu sita uliotolewa,mahakamani imemhuona na hatia ya makosa manne ambapo alimuhukumu kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya sh 700,000.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Rusema alisema kuwa,Mahakama imemkuta na katika makosa yote manne na kwa kosa la kwanza na la pili alitakiwa alipe faini ya sh 250,000 kwa kila kosa ambayo ni sawa na sh 500,000 au kwenda jela miaka miwili na katika shitaka la tatu na la nne alitakiwa kulipa faini ya sh 100,000 au kwenda jela mwaka mmoja.

Chenge alifikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na mashitaka manne likiwemo la kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha vifo vya wanawake waWili,uharibifu wa mali na kuendesha gari bila kuwa na bima.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA