Wafuasi wa CUF wakiandamana jana eneo la Buguruni Malapa wakielekea Ofisi za Wizara ya Sheria na Katiba kuwasilisisha hoja ya kutaka Kataiba Mpya. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA) |
CHAMA Cha Wananchi (CUF) jana kiliwazidi ujanja polisi waliokuwa wakidhibiti maandamano Katika maandamano hayo yaliyosimamisha kwa muda shughuli za kiuchumi na kijamii, wafuasi na wapenzi wa chama hicho wakiongozwa na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro, walifanikiwa kuingia barabarani na kuwasilisha rasimu Kabla ya kuanza maandamano hayo, polisi waliwatangazia wananchi hali ya hatari na kuwataka wajifungie majumbani mwao huku wakifyatua risasi za moto na kurusha mabomo kuwatawanya. Gazeti hili lilifika Buguruni Sheli saa 2:00 asubuhi na kukuta eneo Ilipofika saa 3:30 asubuhi lilipita gari la matangazo la CUF lenye vipaza sauti na ndani yake kulikuwa na mtu aliyekuwa akitangaza kuwa maandamano yapo palepale na yataanzia Makao Makuu ya Chama, saa 4:30 asubuhi badala ya Buguruni Sheli. Mara baada ya tangazo Tafadhali fuateni sheria kuwasilisha madai yenu.” Kauli hiyo ya Dereva wa gari la Polisi aina ya Defenda aliyevalia sare za FFU ilirudiwa mara tatu lakini, wanachama hao hawakusikia badala yake wakaendelea na azma ya kutaka kuandamana huku wakiimba, “Chinja ua, Katiba Lazima.” Tangazo “Mara ya mwisho, narudia wananchi wa CUF maandamano yenu si halali, fuateni sheria kuwasilisha madai yenu,” alisema dereva huyo ambaye jina wala nambari yake haikujukana huku wanachamahao hao wakimjibu, “Hamtufanyi lolote ninyi. Baadaye waandamanaji walianza maandamano na walipofika Rozana, magari ya polisi yaliondoka na kwenda kuegeshwa katika kituo cha mabasi cha Buguruni Malapa, ambako gari maalumu la kumwaga maji ya kuwasha maarufu Salim Said na Elias Sichalwe Lakini, walipofika Malapa, walikumbana na kizuizi cha magari ya polisi zaidi ya sita ya FFU na deraya nyingine. Hapo ilikuwa Wakiwa wanatunishiana misuli katika kituo cha mabasi cha Malapa, gari moja la FFU lilikaa katikati ya barabara na dereva wake alitangaza tena “Tafadhali hili gari usilipite, ukilipita hili gari unatafuta shari.” Lakini pamoja na tangazo Wakati hayo yakiendelea, daladala na magari yote yanayotoka na kwenda Buguruni yalikuwa yamezuia kupita na kupaki pembeni ama kwa amri au kwa hofu Maandamano yalipofika kati ya mitaa ya Ilala Boma na Karume, polisi hao ambao walikuwa tayari wameshajawa na hasira kwa mchezo wa sinema waliokuwa wakichezewa na waandamanaji, waliamua kufyatua risasi za moto kuwatawanya. Pia mabomu kadhaa ya kutoa machozi yalilipuliwa katika mitaa hiyo jambo ambalo lilisababisha waandamanaji hao kuanza kupoteza mwelekeo huku baadhi ya viongozi wao, wakifanikiwa kupita kwa gari la chama lenye bendera. Baadaye maandamano hayo yalifanikiwa kufika ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria ambako viongozi wa CUF walikabidhi rasimu “Tumefanikiwa kufikisha ujumbe wetu ingawa maandamano yetu yalikatiswa na polisi hali ambayo inaonyesha wazi ubakaji wa demokrasia nchini kwani maandamano ni haki ya kikatiba ya kila raia,” alisema Mtatiro. “Tumekabidhi rasimu yetu sifuri ya katiba wizarani, ingawa waziri hatukumkuta lakini tunashukuru imepokewa na katibu mkuu wa wizara hiyo,” aliongeza Mtatiro. Hata hivyo katika makabidhiano ya rasimu hiyo, waandishi wa habari hawakuruhusiwa kuingia ndani ya ofisi na kushuhudia. Mwisho Juzi Kamanda wa Kanda Maalumu ya |
Comments