PIKIPIKI ZISIZO NA VIWANGO MWISHO JAN 31

pikipiki

SERIKALI  imetangaza kwamba itazuia uingizaji wa pikipiki na bajaji zilizotengenezwa chini ya viwango ambazo hazijafikia ubora wake na Shiriki la Viwango nchini (TBS) ifikapo Januari 31 mwaka huu.
Pia imewataka waagizaji na watengenezaji wa pikipiki (Bajaji na Bodaboda) kuhakikisha ubora wa viwango vya pikipiki hizo TBS na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), ili kuhakikisha usalama wa waendesha pikipiki na watuamiaji.
"Watengenezaji na waagizaji wote wa pikipiki wanatakiwa kuhakikisha ubora wa pikipiki zao umethibitishwa na TBS kabla ya Januari 31, 2011. Baada ya muda huo kuisha, pikipiki ambazo hazijathibitishwa ubora na TBS hazitaruhusiwa," imesema sehemu ya taarifa ya  TBS na TRA katika vyombo vya habari jana.
Hatua hiyo ya serikali ni sehemu ya mikakati ya kupunguza ajali nchini ambazo nyingi zimeelezwa kusababishwa na pikipiki maarufu kama bodaboda pamoja na bajaji.
Takwimu za mwaka uliopita wa 2010 zinaonyesha kuwa katika mwaka huo pikipiki zilisababisha ajali 4,471 zilizosababisha vifo, ulemavu, majeraha kwa watu pamoja na kuharibu mali.

Kwa mujibu wa tangazo la serikali kupitia TBS, pikipiki na bajaji ambazo hazitathibitishwa ubora wake hazitaruhusiwa kutembea barabarani ifikapo Januari 31 mwaka huu wala kusajiliwa na TRA.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo pikipiki zote ambazo zitakuwa hazijithibitishwa ubora wake hazitaruhusiwa kuingia kwenye soko la Tanzania na kwamba TRA itatekeleza marufuku hiyo.
"Pikipiki zote ambzo hazijathibitishwa ubora na TBS hazitaruhusiwa kuingia katika soko la Tanzania na marufuku hii itatekelezwa na TRA kupitia idara ya Forodha," imeongeza taarifa hiyo.
 “Viwango vya pikipiki ni vya lazima kwa watengenezaji na waagizaji,viwango hivi vinatoa matakwa ya ubora na usalama wa pikipiki za magurudumu mawili pamoja na zile za magurudumu matatu ambazo zina injini za (Fourstroke),”inasema sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ilifafanua kuwa, matakwa ya ubora wa pikipiki yamebainishwa kwenye viwango ambavyo ni pikipiki zilizopo kwa ajili ya matumizi ya jumla sehemu ya kwanza na sehemu ya pili.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO

TOFAUTI YA WATU WA DAR NA WA MKOANI NI HUU

IBENGE: YANGA SC WATAFUZU HATUA YA ROBO FAINALI.

NILIYOYABAINI KATIKA TRENI YA SGR DAR ,MORO HADI DODOMA … KADOGOSA REKEBISHENI MAMBO HAYA MTANIKUMBUKA