KIZAZAA ZAA CHA MABOMU DAR

Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakipita kuwatambua ndugu zao waliohifadhiwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, baada ya kupoteana wakati wa milipuko ya mabomu  iliyotokea juzi usiku katika Kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ)  namba 511 Gongo la Mboto.


Msafara wa wakazi wa Gongo la Mboto na vitongoji jirani, ukiwa eneo la Banana, Dar es Salaam, ukielekea mjini, kuhofia milipuko ya mabomu.



Mtoto akiwa na mzigo alipokuwa akikimbia mabomu jana.


Rais Jakaya kikwete (katikati), akiwa na huzuni alipokwenda Kambi ya JWTZ , Gongo la Mboto kuangalia ghala namba 5 ambamo mabomu yalilipuka.Kutoka kushoto ni Mkuu wa Majeshi, jenerali Davis mwamunyange, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick na Mkuu wa Kambi ya  JWTZ , Gongo la Mboto,Kanali Aloyce Mwanjile.

Mabomu yakiwa kwenye gari la Polisi, baada ya kukusanywa katika makazi ya watu eneo la Majohe, Dar es Salaam jana

Gari alilopanda Rais Jakaya Kikwete likipita jana eneo la Banana mbele ya lori lililobeba wananchi waliokuwa wakikimbia milipuko mabomu.  iliyotokea juzi usiku katika Kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ)  namaba 511 Gongo la Mboto. Rais Kikwete alikuwa anakwenda kwenye kwenye kambi hiyo kuangalia chanzo cha milipuko.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

TOFAUTI YA WATU WA DAR NA WA MKOANI NI HUU

CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO

IBENGE: YANGA SC WATAFUZU HATUA YA ROBO FAINALI.

NOTI MPYA KUANZA KUSAMBAZWA MWEZI UJAO

HUYU NDIYE DKT. NCHIMBI, MAKAMU WA RAIS AJAE

CHAKUHAWATA WANENA MAKUBWA--