Meneja Masoko wa Kampuni ya Coca-Cola Tanzania, Christina Maina (katikati), akimkabidhi Luninga aina ya Soni, Mwandishi wa habari wa Kampuni ya Guardian, Renatha Msungu, aliyoshinda katika mchezo wa bahati nasibu ya papo kwa papo, iliyochezwa na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kwenye uzinduzi wa kampeni kubwa ya masoko inayoitwa 'Open Happiness' uliofanyika Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Mkazi wa Kampuni hiyo, Dimeji Olaniyan
WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO
WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe amepiga marufuku wasiosomea masuala ya Kilimo kuuza pembejeo. Amesema kuwa masharti ya muuza pembejeo lazima awe amesomea Kilimo kwa ngazi ya cheti, diploma na Digrii. Ameyasema hayo alipokuwa anazungumza na wadau wa mbegu katika mkutano uliofanyika jijini Dodoma. "Haiwezekani wanaowashauri na kuwauzia mbegu wakulima wasiwe na utalaamu wa sekta hiyo, mbona wanaogawa dawa na kutibu wagonjwa wamesomea ufamasia, uuguzi na udaktari, kwa nini isiwe kwenye Kilimo? Amehoji Waziri Bashe. Amewapa kipindi cha mpito cha mwaka mmoja wauzaji kwenda kusomea Kilimo ili waruhusiwe kisheria kuuza Pembejeo na kwamba baada ya hapo sheria itafuata mkondo wake kwa kukagua maduka yote ya pembejeo na kuwakamata watakaobainika.
Comments