MBUNGE DKT. MAJULE ATOA MSAADA WA VYAKULA, VYANDARUA 100 SHULE YA VIZIWI DODOMA

Mbunge wa Viti Maalumu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Dodoma, Dkt. Neema Majule (katikati) ametoa  msaada wa vyakula, vinywaji, vifaa vya usafi na vyandarua 100  kwa  Shule ya Viziwi Dodoma, katika tukio lililofanyika Februari 21, 2026 katika shule hiyo iliyopo Kisasa jijini Dodoma.

Katika tukio hilo, Dkt. Majule ambaye yupo mstari wa mbele  kujitotea kwa hali na mali katika masuala ya kijamii na hasa kwa watu wenye  uhitaji maalumu, alitoa mchele, unga, mafuta, sukari, vinywaji, sabuni, fagio, kalamu, madaftari na pedi kwa ajili ya mabinti.

Kabla ya makabidhiano ya msaada huo, Dkt. Majule alipata wasaa wa kutembelea na kujionea jinsi wanafunzi wanavyopata mafunzo kwa njia ya vitendo ikiwemo ushonaji, kompyuta, ufundi umeme na uselemala lakini pia mchezo wa pooltable.

Mkuu wa shule hiyo, Awadhi Mbogo alitoa shukrani kwa kitendo cha mbunge huyo kuamua kutoa msaada huo mkubwa kwa shule hiyo na kwa aendelee na moyo huo wa kujitolea na kutoa wito kwa wananchi wengine kuiga mfano huo.

Shule hiyo ambayo ni ya serikali, chini ya Manispaa ya Dodoma inasimamiwa pia kwa msaada wa Robin Donker Sgoed ambaye ni Mwasisi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Environmental Oriented  and Training Support (EOTAS).
Dkt. Majule akikabidhi vyakula.


Dkt. Majule akigawa vyandarua hivyo kwa wanafunzi.


Madaftari.
 
Vifaa vya usafi.


Dkt. Majule akigawa vinywaji.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Dodoma, Zainab Mtoro akisaidia kugawa vinywaji.


Wanafunzi wakifurahia vinywaji hivyo.
Wanafunzi wa darasa la kompyuta.


Dkt. Majule akiwaaga wanafunzi.


IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA- 0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

IRAN YAMTANGAZA AYATOLLAH MPYA

Wasifu wa Kizza Besigye

KWA KHERI MAKARANGA UMEUTIMIZA MWENDO...

KWA NINI MAASKOFU JANA KWENYE IBADA YA KUMUAGA PENGO WALIVAA MAVAZI MEUPE WAKATI NI MSIBA..?

DKT. MAJULE AKABIDHIWA CHETI CHA SHUKRANI UWT DODOMA KUFANIKISHA USHINDI WA CCM 2025

WANAOTAZAMWA KUMRITHI AYATOLLAH ALLY KHAMENEI.

MATUKIO RAIS, AMIRI JESHI MKUU DKT. SAMIA AKIZINDUA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA (MMUT)