KWA KHERI MAKARANGA UMEUTIMIZA MWENDO...

#TANZIA: Mwandishi na mhariri mkongwe nchini, Revocatus Makaranga, amefariki dunia Machi 5, 2026 muda mfupi baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa ndugu wa karibu wa familia, Makaranga alikimbizwa katika kitengo cha dharura cha hospitali hiyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu baada ya kuugua ghafla.

Inaelezwa kuwa licha ya jitihada za madaktari kumhudumia, alifariki muda mfupi baada ya kuwasili hospitalini.

Marehemu Makaranga anakumbukwa kama mmoja wa waandishi na wahariri waliotoa mchango mkubwa katika kukuza na kuimarisha tasnia ya habari nchini Tanzania kwa miongo kadhaa. Katika maisha yake ya uandishi, aliwahi kufanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari vya umma wakati wa mfumo wa chama kimoja na baadaye katika kipindi cha mfumo wa vyama vingi.

Aidha, aliwahi pia kufanya kazi katika vyombo vya habari vya sekta binafsi, ikiwemo kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) na New Habari (2006) Ltd, ambako alihusika katika shughuli za uandishi na uhariri wa habari.

Kitaaluma, marehemu Makaranga alikuwa na shahada ya uzamili katika uandishi wa habari aliyoipata kutoka Chuo Kikuu cha Cardiff, Wales, nchini Uingereza.

Taarifa zaidi kuhusu msiba, ikiwemo ratiba ya mazishi, zinatarajiwa kutolewa baadaye na familia.
#ripmakaranga
#MtanzaniaDigital



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

IRAN YAMTANGAZA AYATOLLAH MPYA

Wasifu wa Kizza Besigye

KATI YA WATOTO 7 WA HAYATI MAGUFULI ANAYEJULIKANA ZAIDI NI JESCA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

KIKOSI KILICHOITWA TAIFA STARS HIKI HAPA

KWA NINI MAASKOFU JANA KWENYE IBADA YA KUMUAGA PENGO WALIVAA MAVAZI MEUPE WAKATI NI MSIBA..?

WANAOTAZAMWA KUMRITHI AYATOLLAH ALLY KHAMENEI.

KIJANA WA KINYAKYUSA WA ENZI HIZO, NUSURA AMCHAPE WAZIRI MUONGO BUNGENI