Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda, akitangaza udhamini wa SBL wa Sh. miliono 80, kwa Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA) kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za mwanamichezo bora wa mwaka, Dar es Salaam. Akizungumzia sherehe hiyo, Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto (wapili kushoto) alisema zitafanyika Mei 6, mwaka huu katika jijini, na mshindi wa kwanza atajitwalia gari lenye thamani ya sh. milioni 13. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando, Mjumbe wa TASWA, Masoud Sanani na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TASWA, Maulid Kitenge.
WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO
WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe amepiga marufuku wasiosomea masuala ya Kilimo kuuza pembejeo. Amesema kuwa masharti ya muuza pembejeo lazima awe amesomea Kilimo kwa ngazi ya cheti, diploma na Digrii. Ameyasema hayo alipokuwa anazungumza na wadau wa mbegu katika mkutano uliofanyika jijini Dodoma. "Haiwezekani wanaowashauri na kuwauzia mbegu wakulima wasiwe na utalaamu wa sekta hiyo, mbona wanaogawa dawa na kutibu wagonjwa wamesomea ufamasia, uuguzi na udaktari, kwa nini isiwe kwenye Kilimo? Amehoji Waziri Bashe. Amewapa kipindi cha mpito cha mwaka mmoja wauzaji kwenda kusomea Kilimo ili waruhusiwe kisheria kuuza Pembejeo na kwamba baada ya hapo sheria itafuata mkondo wake kwa kukagua maduka yote ya pembejeo na kuwakamata watakaobainika.
Comments