KESI YA BEN ALI YAANZA LEO


Aliyekuwa Rais wa Tunisia Ben Ali
Kesi ya Rais wa Tunisia aliyeondolewa madarakani Zine al-Abidine Ben Ali imeanza kusikilizwa bila ya yeye kuwepo mahakamani, siku moja baada ya kukanusha madai yote dhidi yake.
Bwana Ben Ali alikimbilia Saudi Arabia Januari 14 kufuatia mapinduzi ya kiraia.
Iwapo atakutwa na hatia atakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 20 jela kutokana na tuhuma mbali mbali ikiwemo rushwa na uuzaji wa dawa za kulevya.
Wanasheria wake wanasema kesi yake ilikuwa ni njama za serikali ya mpito ya Tunisia kupumbaza watu wasiihoji kwa kushindwa kurejesha utulivu na utengamano wa nchi
Mamlaka ya Saudia haijajibu chochote kuhusu ombi la Tunisia kuwa Bwana Ben Ali na mkewe Leila Trabelsi warejeshwe Tunisia na kuna dilili kidogo za wao kuletwa mbele ya mahakama
kukutana na mkono wa sheria.
Mamlaka ya Tunisia imekuwa ikitayarisha mashtaka kadha ya kisheria dhidi ya Ben Ali, lakini kusikilizwa kwa kesi yake Jumatatu hii kutaanza na tuhuma dhidi ya pesa, silaha na dawa za kulevya,
ambazo anatuhumiwa kuziacha katika kasri lake kabla hajakimbia

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA