𝗠𝗮𝗸𝗮𝗯𝗶𝗹𝗮 10 𝗮𝗺𝗯𝗮𝘆𝗼 𝘂𝗸𝗶𝗸𝗮𝗮 𝗸𝗮𝗿𝗶𝗯𝘂 𝗻𝗮𝗼, 𝗸𝘂𝘁𝗼𝗯𝗼𝗮 𝗸𝘂𝗻𝗮𝘄𝗲𝘇𝗮 𝗸𝘂𝘄𝗮 𝗿𝗮𝗵𝗶𝘀𝗶 𝘇𝗮𝗶𝗱𝗶 ⚠️ Kumbuka: Haya ni maoni na mitazamo ya kijamii tu, si kwamba kabila fulani lina mafanikio kuliko lingine. Mafanikio yanategemea juhudi, elimu, nidhamu na fursa. 1. Wasukuma Wana sifa ya kufanya kazi kwa bidii, hasa kwenye kilimo, ufugaji na biashara. Wengi huaminika kuwa wavumilivu katika kutafuta maendeleo. 2. Wachagga Hujulikana kwa moyo wa biashara, uwekezaji na kusaidiana kifamilia katika shughuli za maendeleo. 3. Wahaya Wana historia ndefu ya biashara, elimu na shughuli za uzalishaji zinazochochea maendeleo. 4. Wanyakyusa Wengi wanasifiwa kwa bidii katika biashara, kilimo na uwekezaji wa muda mrefu. 5. Wakinga Hujulikana kwa uchapakazi, nidhamu na uthubutu wa kutafuta fursa sehemu mbalimbali za nchi. 6. Waha Wana sifa ya kujituma katika biashara na shughuli mbalimbali za kiuchumi. 7. Wapare Mara nyingi husifiwa kwa kuthamini elimu, kazi na mipango y...
HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI
MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA
1. Wahiraki, Hawa ni wanawake wa jamii ya Wahiraki wa napatikana kaskazini mwa Tanzania wamezagaa mikoa ya manyara ni weupe Wana Umbo zuri wanavutia kwa Macho. 2. Warangi, Hawa ni wanawake jamii ya Warangi ni wazuri nywele zao ni asili ya waraabu weupe sura nzuri wanapatikana kondoa. 3. Wanyiramba. Hawa ni warembo Sana sura matata wanapatikana mkoa wa singida kaskazini, usipokua makini utawafananisha na wanyaturu 4. Wamasai, kabila hili wanawake wazuri sio wengi Sana lakini ukikutana na sampuli Tatu au nne hivi utauza hata boxa kuongezea mahari wamezagaa Sana Arusha 5. Wahaya, hawa nao ni jamii ya Kanda ya ziwa maumbile Yao Kuna weupe miguu Yao ya bia shape matata wamejaa Sana bukoba. 6. Wanyaturu, Hawa wanafanana na Wanyiramba wanapatikana singida hasa ikungi na manyoni weupe wanavutia 7. Wapare, Hii ni jamii ya kabila la Wapare wanapatikana moshi wilaya ya same wako vizuri usicheze kabisa na hili kabila shape nzuri. 8 .Wamakonde, ...
DK MAGUFULI ATANGAZA KIAMA CHA MAJAMBAZI, WEZI NA MAFISADI KATIKA MIKUTANO YA KAMPENI SUMBAWANGA,TUNDUMA, ILEJE NA MBOZI
DK MAGUFULI ATANGAZA KIAMA CHA MAJAMBAZI, WEZI NA MAFISADI KATIKA MIKUTANO YA KAMPENI SUMBAWANGA,TUNDUMA, ILEJE NA MBOZI on August 26, 2015 Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, John Pombe Joseph Magufuli akihutubia katika mkutano wa kampeni alipokuwa akijinadi leo kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma, wilayani Momba, Mkoa wa Songwe. Magufuli aliseama kuwa endapo akishinda urais atahakikisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Kidato cha Nne wanasoma bila kulipa ada yaani bure. Pia alisema barabara inayoingia mpakani kutoka Mbozi itajengwa njia nne tena kwa kiwango cha lami ili kupunguza msongamano wa magari yanayovuka kwenda Zambia. Dk. Magufuli amesema kuwa akiingia madarakani atahakikisha wezi, majambazi na mafisadi wanaswekwa gerezani. Pia anataka Jeshi la Polisi lenye nidhamu na lenye uwezo wa kupambana na wahalifu wakiwemo majambazi. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG. Dk. Magufuli ...
UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MSALATO DODOMA KUANZA KUTUMIKA SEPTEMBA 2026
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (katikati), akimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Godfrey Kasekenya (Mb) (kulia) kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato jijini Dodoma, ambao unatarajiwa kukamilika na kuanza kutumika mwezi Septemba mwaka huu, hatua inayotarajiwa kuimarisha usafiri wa anga na kulipa hadhi zaidi jiji la Dodoma ambalo ni Makao Makuu ya nchi. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour (wa pili kulia) Na Benny Mwaipaja, Dodoma Serikali imesema kuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato jijini Dodoma unatarajiwa kukamilika na kuanza kutumika ndani ya mwezi Septemba mwaka huu, hatua inayotarajiwa kuimarisha usafiri wa anga na kulipa hadhi zaidi jiji la Dodoma ambalo ni Makao Makuu ya nchi. Akizungumza wakati alipotembelea na kuona maendeleo ya mradi huo, Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), alisema uje...
BALOZI WA CHINA KUPITIA DKT. MAJULE APELEKA NEEMA KWA WANAWAKE DODOMA
Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian amekabidhi msaada wa cherehani 120 kwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa Mkoa huo, Dkt. Neema Majule kwa ajili ya kuzigawa kwa wanawake wa Dodoma Mei 27, 2026. Balozi Mingjian na Dkt. Majule wametiliana saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano baina ya wanawake wa China na wanawake wa Mkoa wa Dodoma katika hafla iliyofanyika Ofisi za Mbunge huyo zilizopo Shule ya Rhema mkoani humo. Akizungumza katika hafla hiyo, Balozi Mingjian amesema China itaendelea kuimarisha ushirikiano wake na Tanzania hususan katika kuwawezesha wanawake na kuongeza fursa za maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Ameeleza kuwa uhusiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na China umeendelea kuleta manufaa kwa wananchi wa mataifa hayo mawili, huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kuinua maisha ya wanawake. Kwa upande wake, Dkt. Majule ameishukuru Serikali ya China kwa msaada huo akisema cherehani h...
VIONGOZI BORA BARANI AFRIKA KWA SASA.
Anaandika Edo Kumwembe Mwandishi na Mtangazaji wa Wasafi TV na Radio. Kutaja viongozi bora barani Afrika kwa sasa kunategemea sana vigezo vinavyotumika kama ni ukuaji wa kiuchumi, Mageuzi ya kidemokrasia, Diplomasia ya kimataifa au ushawishi wa kisiasa. Kulingana na tathmini mbalimbali za kijamii na kisiasa, hawa hapa ni baadhi ya viongozi wanaotajwa sana kwa kuwa na mchango mkubwa na ushawishi mkubwa hapa barani Afrika: 1. Bassirou Diomaye Faye (Senegal) 🫵🏿Kigezo cha Sifa: Demokrasia na Matumaini ya Vijana. Tangu aingie madarakani baada ya kutoka gerezani, Faye amekuwa alama ya demokrasia na uongozi unaoendeshwa na vijana barani Afrika. Amefanya mageuzi makubwa katika mifumo ya kodi, Uwazi wa mikataba ya rasilimali na kurudisha imani ya kiutawala kwa wananchi. 2. Samia Suluhu Hassan (Tanzania) 🫵🏿Kigezo cha Sifa: Diplomasia, Miundombinu, na Ufunguzi wa Uchumi. Rais Samia Suluhu Hassan, Amepongezwa kimataifa kwa falsafa yake ya 4R (Reconciliation, Resilience, Reforms, and...
TUWARASIMISHE BODABODA, WACHANGIE KILA SIKU SH. 1000 -MWALUNENGE
RAIS SAMIA AMTEUA UMMY MWALIMU KUWA MSHAURI WAKE
SERIKALI YAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO NA DIT KUIMARISHA USIMAMIZI WA MAAFA
NA MWANDISHI WETU SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) imeingia Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) yenye lengo la kuimarisha usimamizi wa maafa nchini kwa kutumia sayansi, teknolojia na ubunifu. Akizungumza mapema hii leo (08 Juni, 2026) katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Dkt. Jim Yonazi, amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kujenga mifumo madhubuti ya kiutendaji inayoongozwa na maarifa, sayansi na teknolojia ikiwemo matumizi ya Akili Unde (AI) katika kukabiliana na maafa. Amesema makubaliano hayo yanatekeleza pia mapendekezo ya Mkutano wa Nane wa Umoja wa Mataifa wa Jukwaa la Dunia la Upunguzaji wa Vihatarishi vya Maafa uliofanyika Geneva, Uswisi, mwezi Juni 2025, na yanaashiria mabadiliko ya kimkakati katika namna Serikali inavyoshughulikia changamoto za maafa kuto...
IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA
Pacome Zouzoua alizaliwa tar 30 April 1997 nchini Ivory Coast ktk kitongoji cha Port. Hadi sasa ana umri wa miaka 26, ni kiungo wa kati mwenye uwezo wa kipekee anayetumia zaidi mguu wa kulia ktk kazi yake ya mpira. Alijiunga na Yanga tar 19 - 7 - 2023 majira ya saa 5 usiku akitokea ktk Club ya Asec Mimosas ya nchini Ivory Coast. Ni mchezaji mkakamavu mwenye wepesi miguuni anapokuwana mpira, hujituma sana awapo uwanjani na inavyosemekana ni tofauti sana na awapo ktk mazoezi ya kujiandaa na mechi, lakini siku za mechi kila mara amekuwa moto zaidi nakuwa mkombozi kwa timu kwa kuinasua kimatokeo. Nitaendelea kumpatia maua yake siku zote atakazokuwa ndani ya Young African Sports Club. Pacome Zouzoua anaujuaaaaa.
Comments