VODACOM YAKABIDHI MADAWATI 250 TEMEKE



Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana (kulia)akimpa mkono wa shukurani Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule mara baada ya kukabidhiwa madawati 250 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 22 kwa ajili ya shule za msingi tano za Wilaya ya Temeke,Shule zilizofaidika na msaada huo ni Mgulani,Tandika,Kizuiani,Muongozo,Kilamba,Hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Mgulani jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana akiwasalimu baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Mgulani mara alipofika shuleni hapo kupokea msaada wa madawati 250 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 22 kutoka Vodacom Foundation kwa ajili ya shule za msingi tano za Wilaya ya Temeke,Shule zilizofaidika na msaada huo ni Mgulani,Tandika,Kizuiani,Muongozo,anaeangalia kushoto Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule,Hafla hiyo imefanyika katika shule ya Msingi Mgulani jijini Dar es Salaam.

HABARI KAMILI

KATIKA kuhakikisha inaondoa tatizo la uhaba wa madawati katika shule nchini, kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kupitia mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation, jana ulikabidhi madawati 280 kwa shule mbalimbali za msingi katika Manispaa ya Temeke, yakiwa na thamani ya zaidi ya sh milioni 22.

Makabidhiano hayo ni sehemu ya mpango wa Vodacom Foundation wa kuhakikisha ndani ya wiki moja inakabidhi madawati 500 yenye thamani ya sh milioni 45 kwa shule mbalimbali za msingi katika wilaya za mkoa wa Dar es Salaam ambazo ni Temeke, Ilala na Kinondoni.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa mfuko wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule alisema mradi wa utoaji wa madawati hayo ni sehemu ya kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto wa kitanzania kama nyenzo muhimu ya kuwajengea mazingira bora ya kuja kujisaidia katika maisha yao na kulisadia pia taifa katika fani mbalimbali.

Alisema: “Tunatambua ukubwa wa tatizo na kwamba lipo takribani nchi nzima na tunaguswa nalo, nasi Vodacom kama kampuni yenye kujali maisha ya Watanzania na ndio maana kila mwaka tumekuwa tukiendesha kampeni maalum ya kuchangia madawati ni imani yetu kwamba ipo siku changamoto hii itabakia kuwa historia.”
Alisema kuwa, ukosefu wa madawati nchini ni changamoto inayohitaji nguvu za pamoja baina ya serikali na wadai wakiwamo wa kampuni na taasisi mbalimbali, ili kuwawezesha wanafunzi ambao ndio nguvu kazi ijayo ya taifa kuwa na mazingira bora, salama na rafiki kuwawezesha kufanya vema katika masomo yao.

“Inaumiza sana unapoona watoto wameketi sakafuni au kubanana katika dawati moja darasani, hii lazima itapunguza uwezo wao wa uelewa na ufuatiliaji masomo ndio maana tukaamua kama kampuni inayoungwa mkono na watanzania kuonesha upendo wetu kwa kuwa na kampeni kabambe ya kusaidia madawati mashuleni,” alisema Mwakifulefule.

Makabidhiano ya madawati 280 ni ya awamu ya pili na inazinufaisha shule 11 ambazo ni Mgulani, Tandika, Kizuiani, Mwongozo-Temeke, Kilamba, Maarifa,Kombo, Vingunguti, Mwongozo-Ilala, Kimara B, Kilamba na Ruvu Darajani.

Dhamira ya Vodacom ni kutoa madawati 1,000 yenye thamani ya sh mil. 89 kwa kila wilaya tatu za Dar es Salaam hadi kufikia Oktoba mwaka huu.

Mbali ya mradi wa madawati, Vodacom Foundation imekuwa pia ikisadia uimarishaji na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya shule za sekondari na msingi hapa nchini ikiwemo madarasa, mabweni,maabara, vyoo na kadhalika, katika maeneo ya mijini na vijijini.

Vodacom Foundation ni mfuko uliojijengea heshima kubwa hapa nchini kwa kuwa mstari wa mbele katika kusaidia jamii katika azma ya kubadili maisha ya wananchi kupitia sekta ya elimu,afya, mazingira na ujasiriamali.
Mwisho.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA