ARSENAL YAIFUMUA CHELSEA MABAO 5-3


Mshambuliaji hatari wa Arsenal Robin van Persie amefunga mabao matatu wakati Arsenal ilipoichakaza Chelsea mabao 5-3 katika mchezo wa kusisimua uliochezwa katika uwanja wa Stanford Bridge.Robin van Persie (pichani)

Kiungo wa Chelsea Frank Lampard alikuwa wa kwanza kufungua mlango wa Arsenal kwa bao la kichwa lakini Van Persie akasawazisha muda mfupi.

John Terry akaipatia bao la pili Chelsea kwa mkwaju wa karibu kiasi cha yadi 16 kabla beki Andre Santos kusawazisha kipindi cha pili kwa mkwaju uliompita katikati ya miguu mlinda mlango wa Chelsea Petr Cech.

Theo Walcott aliiongezea uhai Arsenal kwa kufunga bao la tatu baada ya kupenya katika msitu wa mabeki wa Chelsea na Juan Mata baadae akaisawazishia Chelsea kwa kufunga bao la tatu kabla ya Van Persie kuongeza bao la nne katika lango lililokuwa wazi baada ya beki na nahodha wa Chelsea John Terry kuteleza.

Van Persie mabao yake mawili ya mwisho aliyafunga katika kipindi cha dakika tano.

Na baadae mshambuliaji huyo wa Arsenal akichezeshwa na Mikel Arteta kwa pasi murua dakika za nyongeza na akafumua mkwaju mkali ambapo mlinda mlango Petr Cech hakuweza kufanya lolote na kushuhudia nyavu zikicheza na kuiandikia bao la tano.

Ushindi huo umeiinua Arsenal hadi nafasi ya sita katika msimamo wa ligi.

Hernandez

Hernandez

Nayo Manchester United ilizinduka baada ya kipigo cha Jumapili iliyopita cha mabao 6-1 kutoka kwa Manchester City baada ya bao moja alilofunga Javier Hernandez kuwapa mshindi mgumu katika uwanja wa Everton.

Hernandez alitengewa mpira wa krosi kutoka kwa Patrice Evra katika dakika ya 19.

Bao hilo lilikuwa ni zawadi nzuri kutokana na kandanda nzuri waliyocheza United, lakini Everton walikuwa wakiisumbua sana Manchester United katika dakika zote zilizosalia.

Leighton Baines wa Everton alikosa bao baada ya mkwaju wake wa adhabu ndogo kugonga mwamba na mkwaju wa Louis Saha nao hakukuweza kulenga lango.

Matokeo hayo yameiimarisha Manchester United katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kwa kufikisha pointi 23.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA