KONGAMANO LA WANAHABARI JUU YA UTAFITI WA HUDUMA YA AFYA ITOLEWAYO NA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF) NCHINI


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia) akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Emmanuel Humba (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya mfuko huo, Ally Kiwenge (wa pili kushoto) baada ya kufungua kongamano la saba la mwaka la wahariri wa habari na waandishi waandamizi la kujadili taarifa za utafiti wa huduma za NHIF nchini. Kongamano hilo la siku mbili limeanza leo mjini Morogoro.

Mwandishi wa Habari, Joshua Joel akifafanua jambo alipokuwa akitoa katika kongamano hilo taarifa ya utafiti wa upatikanaji wa huduma za afya zitolewazo na NHIF, katika mikoa ya Rukwa na Katavi.
Jennifer Sumi wa gazeti la Mwananchi na Scolastica Mazula wa Redio Times FM, wakiwa katika kongamano hilo

Said Mmanga kutoka gazeti la Changamoto, akitoa taari ya utafiti kuhusu upatikanaji wa huduma za afya vijijini walioufanya na Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, George Marato katika Mkoa wa Mara.


Beda Msimbe wa magazeti ya Serikali ya Daily News na Habari Leo, akitoa taarifa ya utafiti wa huduma zitolewazo na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), katika Mkoa wa Ruvuma.


Mwandishi wa habari mwandamizi wa gazeti la Jambo Leo, Grace Michael akitoa taarifa ya utafiti wa huduma za afya zilitolewazo na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), katika Mkoa wa Kigoma.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia), akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari,baada ya kufungua kongamano la saba la mwaka la wahariri wa habari na waandishi waandamizi la kujadili taarifa za utafiti wa huduma za NHIF nchini. Kongamano hilo la siku mbili lilianza mjini Morogoro.


Baadhi ya wahariri wa habari na waandishi waandamizi wakiwa katika kongamano la saba la mwaka la kujadili taarifa za utafiti wa huduma za NHIF nchini, lililoanza jana mjini Morogoro.


Wachora vibonzo Nathan Mpangala (kulia) na King Kinya wakisikiliza kwa makini wakati wa kongamano likiendelea.


Baadhi ya wahariri wa habari na waandishi waandamizi wakiwa katika kongamano la saba la
mwaka la kujadili taarifa za utafiti wa huduma za NHIF nchini, lililoanza jana mjini Morogoro.

Beda Msimbe wa magazeti ya Serikali ya Daily News na Habari Leo, akitoa taarifa ya utafiti wa huduma zitolewazo na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), katika Mkoa wa Ruvuma.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA