FILAMU YA MR PRESIDENT YAZINDULIWA DAR

Vick Kamata mbunge wa Viti Maalum CCM ambaye ndiye Mgeni rasmi katika uzinduzi wa filamu ya Mr. President uliofanyika usiku huu kwenye hoteli ya Serena Dar es salaam, akiizinduzi filamu hiyo ambayo inaelezea maisha ya kiongozi wa nchi . Mbunge Vick Kamata amewaeleza wasanii mbalimbai waliohudhuria katika uzinduzi huo kuwa anaimani kuwa sheria mpya ya haki miliki itatungwa na Bunge ili kulinda kazi za wasanii kutokana na kuibiwa kazi zao muda mrefu. Ameongeza kwamba kazi ya sanaa ni kazi nzuri ambayo imekuwa ikiwasaidia wasanii kuishi maisha mazuri, lakini pia kufanya maendeleo katika maisha yao.
Vick Kamata amezindua filamu hiyo kwa niaba ya Waziri Mathias Chikawe ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo hata hivyo hakuhudhuria kutokana na majukumu mengine ya kitaifa


Steve Mengele aka Steve Nyerere akitambulisha waigizaji wenzake wal;ioshiriki katika filamu ya Mr. President ambayo yeye mwenyewe ameigiza kama Rais katika filamu hiyo, huku waigizaji wenzake wakonekana wenye furaha katikauzinduzi huo. PICHA KWA HISANI YA FULL SHANGWE BLOG



Wsanii mbalimbali walioshiriki kuigiza filamu ya Mr. President wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi huo.






Bendi ya Borabora Sound ikitumbuiza katika uzinduzi huo kwenye hoteli ya Serena Dar es salaam.








Wageni mbalimbali wakiwa katika uzinduzi wa filamu hiyo.










Wazee wa mpira kutoka kulia ni Evans Aveva akiongea na Charles Hamka, Mohamed Nasor, Philemon pamoja na Juma Pinto wakishiriki katika uzinduzi huo.











Comments

Anonymous said…
Kamanda filamu hiyo inapatikana wapi?

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA

DKT NCHIMBI AZURU KABURI LA JOHN KOMBA LITUHI, NYASA

DKT NCHIMBI AAGIZA UJENZI UWANJA WA NDEGE SUMBAWANGA UKAMILIKE HARAKA