HEKAHEKA WATAKAOHAMIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO

Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kijiji cha Mabwepande, Omar Ally, akizungumza na wakazi wa kijiji hicho, mara baada ya mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana alioufanya kijijini hapo, kuhusu kuachia maeneo yao kwa ajili ya kupewa watu waliokubwa na mafuriko wa Wilaya hiyo. Hata hivyo katika mkutano wao huo, wakazi hao, hawakukubalina na suala la kuyaachia maeneo yao hayo.
Ofisa Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, akipima viwanja vitakavyogawiwa kwa waathirika wa mafuriko wa mabondeni, katika eneo la Mabwepande, Kinondoni, Dar es Salaam.


wakazi wa eneo hilo la Mabwepande wakiendelea na ujenzi wa nyumba.

Baadhi ya wamiliki wa mashamba wakiwa eneo hilo kufuatilia hatima mgogoro huo.
Augustino Mrosso akionesha kibanda chake alichojenga kwenye shamba lake lililopo katika eneo la Mabwepande, linalotarajiwa kugawiwa kwa waathirika wa mafuriko mabondeni, Dar es Salaam.
Vijana wakiwa wamebeba matofali ya kujengea nyumba katika moja ya viwanja katika eneo hilo.
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo la Mabwepande wakiendelea na ujenzi wa nyumba, huku kukiwepo taarifa za eneo hilo kupimwa na kugawiwa kwa waathirika wa mafuriko.
Mmoja wa maofisa Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, akiwa amebeba moja ya vifaa vya kazi wakati wa mchakato wa upimaji wa viwanja vitakavyogawiwa kwa waathirika wa mafuriko wa mabondeni, katika eneo la Mabwepande, Kinondoni, Dar es Salaam.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA