JK AMWAPISHA OMBENI SEFUE KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI

Rais Jakaya Kikwete akimuapisha Balozi Ombeni Sefue kuwa Katibu Mkuu Kiongozi leo Ikulu Dar es salaam.

Katibu Mkuu Kiongozi aliyemaliza muda wake, Philemon Luhanjo (kulia) akimpongeza aliyechukua nafasi yake, Ombeni Sefue wakati wa hafala hiyo




JK akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi mpya Sefue (wa tatu kushoto mstari wa mbele), pamoja na viongozi wengine

MJUE KATIBU MKUU MPYA KIONGOZI

KATIBU Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue ni mwanataaluma ya diplomasia ambaye tokea Agosti 31, 2010 amekuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani.

ya kuteuliwa kwenda Umoja wa Mataifa, Balozi Sefue alikuwa Balozi wa Tanzania katika Marekani mjini Washington DC tokea Juni 15, 2007. Na kabla ya hapo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada nafasi aliyoishikilia kati ya Oktoba 2005 hadi Juni 2007.

Balozi Sefue amekuwa mtumishi wa Serikali tokea 1977 alipoajiriwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa Ofisa wa Mambo ya Nje. Alipanda nafasi Serikalini na kati ya mwaka 1987 na 1992 Bw. Sefue alikuwa Ofisa Mwandamizi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden Mjini Stockholm.

Kati ya mwaka 1993 na 2005, Bwana Sefue alikuwa mwandishi wa hotuba na msaidizi binafsi wa marais wawili – Rais Ali Hassan Mwinyi (1993-1995) na Rais Benjamin William Mkapa (1995-2005).

Miongoni mwa mambo mengine, Balozi Sefue alimsaidia Rais Mkapa wakati Rais alipokuwa Kamishna wa Afrika (Kwenye Kamisheni ya Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo – Mhe. Tony Blair) ambayo ilitoa ripoti iitwayo, Our Common Interest: Report of the Commission for Africa mwezi Machi mwaka 2005, na alishiriki naye kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za G8 ambao ulijadili ripoti hiyo na uliofanyika Gleneagles, Scotland mwezi Julai mwaka 2005.

Balozi Sefue pia alifanya kazi na Rais Mkapa wakati Mheshimiwa Mkapa alipokuwa Mwenyekiti Mwenza wa Kamisheni ya Shirika la Kazi Duniani ya ILO World Commission iliyojadili Masuala ya Kijamii ya Utandawazi kati ya mwaka 2002 na 2004 ambako alishiriki katika maandalizi ya ripoti ya kamisheni hiyo iitwayo A Fair Globalisation: Creating Opportunities For All, iliyotolewa mwezi Februari mwaka 2004.


Balozi Sefue alipata elimu yake ya juu katika Chuo cha Mzumbe (ambacho kwa sasa ni Chuo Kikuu cha Mzumbe) katika masuala ya Utawala mwaka 1977. Alipata Shahada ya Uzamili katika masuala ya Sera na Utawala kutoka Institute of Social Studies (ISS) mjini The Hague, Uholanzi mwaka 1981. Pia alipata diploma ya juu katika masuala ya Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia kutoka Chuo cha Diplomasia cha Dar es Salaam mwaka 1986.


Balozi Sefue amemwoa Mama Anita M. Sefue na wana watoto wawili.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA