MAFURIKO MAKUBWA YAJA TENA DAR

Hali ya Hewa: Mafuriko makubwa yanakuja Dar
YASEMA ALHAMISI HADI JUMAMOSI KUWA SIKU MBAYA ZAIDI, PIA KUYAKUMBA MAENEO MENGINE NCHINIWaandishi wetuMAMLAKA
ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa tahadhari ya kuendelea kunyesha
mvua kubwa zaidi katika siku 10 zijazo, huku ikizitaja Alhamisi hadi
Jumamosi kuwa ni siku za mafuriko mengine makubwa zaidi katika jiji la
Dar es Salaam.Wakati TMA ikitoa tahadhari hiyo, Shirika la Reli
Tanzania (TRL), limesitisha safari za treni ya abiria kwa muda
usiojulikana kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma, kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali ya nchi.Mkurugenzi Mkuu
wa TMA, Dk Agnes Kijazi alisema jana katika taarifa yake kuwa kutokana
na mvua hizo, ni vyema tahadhari zote zikachukuliwa mapema ili kuepuka
maafa zaidi.“Wale wananchi ambao wanaishi mabondeni na
waliokumbwa na mafuriko, wahame kutokana na mvua zinazoanza kunyesha
Desemba 27 (jana), hadi Desemba 31 mwaka huu, kwani zitaleta madhara
makubwa kwa wanaoishi mabondeni na sehemu nyingine mbalimbali,” alisema
Dk Kijazi.Alisema kwamba ukanda wa mvua unatarajia kuimarika
maeneo mengi nchini na mvua zinatarajiwa kuanza kwenye ukanda wa pwani,
ikiwemo Mkoa wa Dar es Salaam na kuongezeka kuelekea mwaka mpya wa 2012.Dk
Kijazi alisema mifumo ya hali ya hewa inaonyesha kuimarika kwa hali ya
joto katika Bahari ya Hindi na kuongezeka kwa msukumo wa hewa yenye
unyevunyevu kutoka misitu ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).Alisema
hali hiyo imesababisha makutano ya upepo katika eneo la Mashariki na
Kusini Magharibi mwa nchi, kuanzia leo kuelekea mwaka mpya... “Hali hii
inatarajia kusababisha kuanza kwa vipindi vya mvua kubwa katika maeneo
mengi hapa nchini.”Alisema maeneo ya mikoa ya ukanda wa Pwani
(Dar es Salaam, Pwani, Mtwara, Lindi na Unguja), yanatarajiwa kuwa na
vipindi vya mvua kubwa.Dk Kijazi aliyataja maeneo mengine kuwa ni
ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi ambayo ni Mikoa ya Mbeya, Iringa na
Rukwa na Kanda ya Kati katika Mikoa ya Dodoma na Singida.“Kwa
upande wa Magharibi mwa nchi, Mikoa ya Kigoma na Tabora na maeneo
machache ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki katika Mikoa ya
Kilimanjaro, Arusha na Manyara, yanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua
kubwa,” alisema.Alisema kutokana na viwango vikubwa vya mvua
vilivyonyesha, ongezeko kidogo la mvua linatarajia kusababisha mafuriko
na uharibifu wa miundombinu, hivyo ni muhimu tahadhari stahili ziendelee
kuzingatiwa.Msimbazi wagomaLicha ya tahadhari hiyo ya TMA,
baadhi ya wakazi waishio katika Bonde la Mto Msimbazi wamedai kuwa
hawataondoka katika nyumba zao zilizokumbwa na mafuriko hadi watakapoona
maji yamejaa katika mto huo.Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti wakazi hao walisema hawana pa kwenda licha ya kuisikia tahadhari hiyo ya TMA.“Ningekuwa
mpangaji sawa, sasa mimi nimejenga nitakwenda wapi na kwetu ni mikoani
huko,” alisema Ramadhani Kimbuyu wakati akifanya ukarabati wa nyumba
yake huku akisisitiza kuwa kipimo chao kitakuwa Mto Msimbazi.Alisema
kosa walilofanya awali ni kupuuza licha ya kuona mto huo umejaa jambo
ambalo alidai hawatalirudia... “Tukiona yamejaa tu tunahamia juu relini,
yakipungua tunarudi.”Kauli ya RCMkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Said Mecky Sadiki amesema Serikali itawachukulia hatua kali
watakaokaidi amri ilivyotangazwa na Rais Jakaya Kikwete ya kutorejea
katika maeneo hatarishi ya mabondeni.“Tangu mwaka 1979 Serikali
ilitoa amri ya watu kuondoka mabondeni lakini wamekuwa wakikaidi na
kuendelea kuishi, kitendo hicho kimechangiwa na uzembe kwa baadhi ya
viongozi katika kutekeleza agizo hilo,” alisema.Sadiki alisema
baadhi ya watu wameanza kurejea kwenye mabonde yaliyoathirika na
kuwaonya wasirudi na badala yake watafute maeneo mengine kuendesha
makazi yao.Alisema Serikali itawapatia waliojenga mabondeni
viwanja na siyo wapangaji. Wakazi hao wametengewa viwanja katika eneo la
Mabwe Pande lililoko mpakani na Bagamoyo, Pwani na kwamba mpaka sasa
viwanja 700 vimeshapimwa.“Baada ya kugawa viwanja hivi tutaanza
zoezi la kuzibomoa nyumba walizokuwa wanaishi maeneo ya mabondeni ili
kutoruhusu watu kurudi tena huko kwani bila kufanya hivyo,
hatutafanikisha lengo hilo,” alisema Sadiki.Treni zatishwaKutokana
na mvua kubwa zinazonyesha maeneo mbalimbali nchini wa TRL, jana
ulitangaza kusitishwa kwa safari za treni ya abiria kutoka Dar es Salaam
hadi Kigoma... “Safari hizo zimesitishwa hadi itakapotangwa vinginevyo
baadaye,” alisema Meneja Uhusiano wa TRL, Midladjy Maez.Alisema
abiria wote waliokuwa wamepanga kusafiri jana na katika treni zijazo,
wanatakiwa kufika na tiketi zao katika ofisi za Stesheni Masta wa kituo
husika ili warejeshewe fedha zao. Walia na huduma mbovuWaathirika
wa mafuriko waliopo katika Kituo cha Hananasifu, Kinondoni Dar es
Salaam, wamelalamikia uongozi wa kituo hicho kutoa huduma za chakula na
malazi usiku bila umeme.Wakizungumza kambini hapo jana waathirika
hao walisema, uongozi unatoa huduma hizo waathirika kuanzia saa 4:00
hadi saa 6:00 usiku kitendo ambacho kinafanya baadhi yao wapoteze vifaa
vyao.Kambi ya Hananasif imeshapoteza magodoro 50, ambayo inaelezwa na
wananchi hao kuwa waliohusika ni baadhi ya viongozi waliopewa dhamana ya
kuhudumia eneo hilo.“Hapa kituoni hatuna umeme, lakini utaona
viongozi wanakaa kimya mpaka ifike saa nne ndipo wanaanza kugawa
magodoro, wengine wakishirikiana na vibaka usiku kuhamisha baadhi ya
magodoro kupeleka mahali kusikojulikana,” alisema Hamed Shaban.Habari hii imeandikwa na Boniface Meena, Keneth Goliama na Aidan Mhando, Pamela Chilongola, Joseph Zablon, Ibrahim Yamola.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA