AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU SEKONDARI YA OSHARA


Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Oshara Elieta Kaaya na wanafunzi
Reina Kileo na Joseph Mwita kwa pamoja wakipokea vitabu toka kwa
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Siha,Bw.Rashid
Kitambulo vilivyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel chini
ya mpango wake wa shule yetu Akishuhudia makabithiano hayo ni Afisa
uhusiano wa Airtel Jane Matinde.katika hafla ya makabidhiano
iliyofanyika shule ya sekondari Oshara
Afisa Uhusiano wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel ,Jane Matinde
akikabidhi vitabu kwa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya
ya Siha,Bw.Rashid Kitambulo,kwa niaba ya shule nne zilizokabidhiwa
vitabu hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni moja kwa kila
shule,shule hizo ni Oshara,Magadini,Kilingi pamoja na shule ya
sekondari ya Namwai,zilizoko Wilaya ya Siha,Mkoani Kilimanjaro,(kulia)
ni Mkuu wa shule ya Sekonri ya Oshara, Bw.Elieta Kaaya pamoja na
meneja mauzo wa Airtel bw. Pascal Bikomagu.hafla hiyo ya makabidhiano
iliyofanyika shule ya sekondari Oshara
Wanafunzi na walimu wa shule za sekondari Oshara, Magadini,Kilingi
pamoja na shule ya sekondari ya Namwai,zilizoko Wilaya ya Siha,Mkoani
Kilimanjaro wakiwa katika halfa ya kukabithiwa vitabu vya kiada
zilivyotolewa na kampuni ya simu ya Airtel chini ya mpango wake wa
shule yetu katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika shule ya
sekondari Oshara
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Siha,Bw.Rashid
Kitambulo akizungumza na kuishukuru kampuni ya Airtel kwa msaada
mkubwa wa vitabu ilioutoa kwa shule nne za sekondari zailizopo
wilayani hapo, mwisho kushoto ni Mwalimu mkuu wa sekondari ya Oshara
Elieta Kaaya akifatiwa na wawakilishi wa Airtel Pascal Bikomagu na
Jane matinde (kulia) ni Afisa Elimu Taaluma wa sekondari Wilaya ya
Siha,Bw. Mussa Shaban Ally.hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika
shule ya sekondari Oshara

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

KANUNI 10 ZA MAHUSIANO YENYE FURAHA

HAKI 13 ZA MWANAMKE LAZIMA MWANAUME AZIHESHIMU:

MAMBO SABA AMBAYO WANAUME WENGI HAWAYAPENDI:

NI HESHIMA KUBWA SANA KUIFUNDISHA YANGA - KOCHA MPYA WA YANGA

RAIS DKT.MWINYI: ZANZIBAR KUWA KITUO CHA BIASHARA CHA KIMATAIFA

”RAIS SAMIA AUMIZWA MAUAJI YA KIBIKI”

KOCHA SEAD RAMOVIC AMRITHI GAMONDI YANGA.

UOKOAJI KARIAKOO NI USHUHUDA WA MOYO WA UTANZANIA: NCHIMBI

ACHENI KUWA CHANZO CHA CHOKOCHOKO NA VURUGU - ASKOFU CHANDE