Basi la New Force likiwa limeharibika vibaya baada ya kugonga nyumba
Mgahawa uliopo Stendi Kuu ya Mbeya ulioparamiwa na basi hilo. (picha na habari kwa hisani ya blogu ya Mbeya Yetu)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhtDwSxwdAWGkZBNC1d6F5GzKl38pkiFdmXGtcET0x24oFKa2ur86oEIRItzxk4Hi_w_Jo5Feqg_xkPDbDduO8FTpd5kxshuHPJ_gCTSg2wVC5iyuTIEsnIQrIm3dLeS7H-q-lidW4nc1M/s640/new+force+T853+avq.JPG)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhNY4JLK07UFShrFchgfuUSN6dz_JxcyVclHCfDNSMUlCAeY5I0-zPx6LqLfUk8NCFOHT1WwbaJ6J5YY2CD05VS3M9Fu8B4QkHRhMjAHouYL6pmcy86PYiQK6ta4Wb1NIoFIBhXiv701ag/s640/ofisi+za+New+Force+stendi+mbeya.JPG) |
ABIRIA
aliyefahamika kwa jina moja la Amina mkazi wa wilaya ya Mbozi mkoani
Mbeya alikufa papo hapo katika ajali iliyotokea juzi usiku katika Kituo
cha Mabasi yaendayo Mikoani kutokea Mbeya baada ya basi la New Force
kuparamia ukuta wa mgahawa uliopo mkabala na Ofisi za Mabasi ya Kampuni
hilo.
Tukio
hilo limetokea majira ya saa 5:00 usiku wa Ijumaa ya Januari 20 mwaka
huu katika Kituo hicho cha Mabasi yakitokea mikoa mingine.
Mashuhuda
wa tukio hilo wamesema kondakta wa basi hilo aliyejulikana kwa jina la
Januari Kapinga aliingia ndani ya basi hilo lenye namba za usajili T 853
AVQ aina ya Yutong lililokuwa likitokea Dar es Salaam baada ya abiria
wote kushuka ndipo alipolikurupua kwa nguvu na kumshinda hatimaye
kuparamia ukuta.
Abiria
aliyefariki alikuwa safarini kuelekea masomoni mkoani Tabora na wakati
gari likiparamia ukuta wa mgahawa huo alikuwa akipata chakula cha jioni
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema licha ya mmoja huyo kupoteza maisha, lakini watano wamejeruhiwa.
Aidha
kondakta wa basi hilo alitoroka na kwenda kusikojulikana na juhudi za
Jeshi la Polis kumtafuta zinaendelea na hadi sasa dereva wa basi hilo
anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano zaidi.
Kwa upande wake Noah Mwakatumbula
Mwenyekiti wa Kituo cha Mabasi mkoani Mbeya yaendayo mikoani amewataka
madereva waliopewa dhamana ya kuendesha vyombo hivyo na serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waache mara moja tabia ya kuacha funguo
za vyombo vyao vya usafiri.
|
Comments