Naibu
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu ameitaka
timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) kuhakikisha inabuka na ushindi
kwenye mechi yake dhidi ya Namibia.
Mechi
hiyo ya kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC)
itachezwa Januari 14 mwaka huu jijini Windhoek, Nambia na timu hizo
zitarudiana Januari 29 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Waziri
ametoa mwito huo leo mchana (Januari 11 mwaka huu) katika hafla fupi ya
kuiaga timu hiyo na kuikabidhi Bendera ya Taifa iliyofanyika ofisi za
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Timu
hiyo yenye msafara wa watu 25 inaondoka leo saa 2 usiku (Januari 11
mwaka huu) kwa ndege ya PrecisionAir kupitia Johannesburg, Afrika Kusini
ambapo kesho alfajiri (Januari 12 mwaka huu) itaunganisha safari hiyo
kwa ndege ya Air Namibia hadi Windhoek.
Wachezaji
walioko kwenye kikosi hicho ni Asha Rashid, Aziza Mwadini, Ettoe
Mlenzi, Fadhila Hamad, Fatuma Bushiri, Fatuma Khatib, Fatuma Mustapha,
Fatuma Omari, Maimuna Said, Mwajuma Abdallah, Mwanahamisi Omari,
Mwanaidi Hamisi, Mwapewa Mtumwa, Pulkaria Charaji, Rukia Hamisi, Siajabu
Hassan, Semeni Abeid, Sophia Mwasikili na Zena Khamisi.
Benchi
la Ufundi lina Kocha Mkuu Charles Boniface, Kocha Msaidizi Nasra
Mohamed, daktari wa timu Dk. Christina Luambano na Meneja wa timu Furaha
Francis.
Kiongozi
wa msafara ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake
Tanzania (TWFA) ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Lina
Mhando na Naibu kiongozi wa msafara ni mjumbe wa Chama cha Soka Zanzibar
(ZFA), Layla Abdallah.
Timu hiyo itarejea alfajiri ya Januari 16 mwaka huu kwa ndege ya PrecisionAir.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
|
Comments