UNITED REPUBLIC OF TANZANIA DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898

E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com

press@ikulu.go.tz

Fax: 255-22-2113425

Coat of Arms

PRESIDENT’S OFFICE,

THE STATE HOUSE,

P.O. BOX 9120,

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Bara la Afrika linakabiliwa na changamoto nyingi katika kuleta mageuzi katika kilimo chake lakini ni muhimu changamoto hizo zinaweza kutatuliwa kwa pamoja kati ya Serikali na Sekta Binafsi.

Rais Kikwete ameeleza hayo katika mkutano wa wadau wa Uchumi wanaokutana mjini Davos-Switzerland, kuzungumzia mageuzi na changamoto za uchumi na fedha zinazoikabili dunia kwa sasa.

Katika Mada inayohusu mtazamo na muelekeo mpya wa Kilimo na hatua zinazoweza kuchukuliwa, Rais kikwete amesema, sekta ya kilimo barani Afrika inahitaji mageuzi makubwa ya kukifanya kiwe cha kisasa na chenye tija na hatimaye kuweza kuzalisha chakula kwa ajili ya matumizi ya watu wake na ziada kwa ajili ya kuuza nje ya bara hilo.

Ukizungumzia mageuzi ya kilimo unazungumzia kilimo kinachotegemea sayansi na teknolojia ya kisasa itakayotufanya tutumie mbolea, mbegu bora, zana bora za kisasa ili kilimo hiki kiwe na tija”. Rais amesema na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo, bara la Afrika litakuwa limewatoa wananchi wake kwenye umaskini mkubwa lakini pia kuongeza ajira na kuvutia maendeleo zaidi Barani Afrika.

Rais amewaeleza wajumbe wa mkutano huo unaojumuisha Viongozi wa Serikali, Wakuu wa Makampuni na Mashirika ya Kibiashara, Kifedha na Wataalamu mbalimbali wa Fedha na Uchumi duniani.

Kilimo barani Afrika pia kimekuwa na changamoto nyingi kutokana na kuwa kinaendeshwa na serikali, mara nyingi serikali zimekuwa zinakabiliwa na upungufu wa fedha hivyo kutenga fedha chache na zisizotosheleza katika kufanya shughuli za utafiti na kuboresha kilimo kwa ujumla”. Rais amesema na kutoa mwito kwa nchi tajiri, wafanyabiashara wakubwa na wadau wa maendeleo kutoa kipaumbele na kuanza kutilia maanani sekta hii ya kilimo barani Afrika.

Tunaweza kushirikisha sekta binafsi ili kuchangia nguvu na mchango wa serikali, kwa pamoja tutaweza kukuza kilimo cha Afrika na kukifanya kiwe na tija zaidi kwa wakulima na wadau wote kwa ujumla”.

Amesema na kutoa mfano wa mkakati wa kukuza kilimo Kusini mwa Tanzania unaohusisha mikoa mitano, iliyo katika ukanda wa Tazara maarufu kama Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT).

Mpango ambao unajumuisha juhudi za Serikali, Sekta Binafsi na Makampuni Binafsi ya nje na ndani ya Tanzania.

Lengo kubwa la mpango huu ni kuzalisha chakula kwa wingi hasa mahindi katika Mikoa ya Iringa, Ruvuma, Mbeya, Rukwa na Morogoro, kwa ajili ya matumizi ya ndani na nje ya Tanzania.

Rais Kikwete ametoa mfano huu wa SAGCOT na kutoa changamoto kwa wadau na washiriki wa Mkutano wa mwaka huu wa Uchumi Duniani, maarufu kama World Economic Forum (WEF), kutumia mpango huu kama mfano wa kuigwa na kutumika katika nchi zingine za Afrika, ili kuboresha na kuleta mabadiliko katika Kilimo barani Afrika na hatimaye, kuchangia katika kukuza uchumi na maendeleo ya bara la Afrika na dunia kwa ujumla.

Rais Kikwete ameondoka leo tarehe 28 Januari 2012, kuelekea Addis Ababa, Ethiopia kuhudhuria kikao cha Wakuu wa Nchi cha kila mwaka.

Mwisho.

Imetolewa na Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais,

Davos-Switzerland.

28 Januari, 2012

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA