Jinsi ya Kutumia mini disc Sony MZ-R55

Kutumia Mini Disc
Jinsi ya Kutumia mini disc Sony MZ-R55

Mindisc recorder hii hutumia minidisks (MDS) kwa kurekodi
kujitayarisha kurekodi

• Kwanza kabisa recorder hii hutumia nguvu (power) ya stima ama umeme kwa njia ya adaptor ya nguvu ya volt 3, inaweza pia kutumia batri za (AA). Njia nyigine ni kwa kutumia batri zinazoweza kujazwa upya nguvu ama rechargeable. Ukitumia batri unaweza kuitumia kwa saa mbili na nusu.

• Ukitumia betri za kujazwa upya nguvu ama rechargeable chomeka adaptor kwenye socket ya umeme ama stima halafu unganishe kwenye mini disc recorder na baadae halafu finya kitufe kinachoonesha STOP/CHARGE button kwenye minidisk, ukiangalia kwenye display utaona picha ya batri ikionyesha kwenye kioo cha display, kama batri ilikuwa imetumika kabisa basi ku-chaji kutachukua kama saa tatu hivi, ni vyema kutumia batri ikiwa imetumika kabisa kabla ya kuanza ku-chaji tena, kwani huogeza wa maisha ya batri hiyo.

Kutumia microphone kwenye minidisk
• Hakikisha kabla ya kuanza kurekodi una minidisk machine, minidisk za kurekodia, batri, microphone na headphones

• Chomeka microphone kwenye tundu au socket iliyo nyekundu kando mwa recorder kwa kutumia cable iliyotengenezwa maalum kutumika na microphone upande mmoja ni xlr (Female) na upande mwingine plug ya 3.5 mm ama mini jack.

• MIC SENS switch kwenye upande mwa recorder iwe switched kwenye HIGH.

• VOLUME inaweza kuongezwa kwa alama ya kujumlisha + na kupunguza kwa alama ya kupunguza –

• Sasa unaweza kuweka minidisk kwenye mashine kwa kutumia open/kufungua kwenye upande wa recorder fungua halafu tumbukiza minidisc hakikisha label ama maadishi yakiangalia juu halafu funga ki-mlango kwa kubonyeza chini.

• Sasa unaweza kurekodi.

• Finya record button kwenye upande wa mashine

• Kwenye kioo au display utaona maadishi yanaonyesha REC na MIC recording level hufanyika kwenye minidisc

• Unaweza kusimamisha kurekodi kwa muda kwa kutumia kitufe cha pause

• Unaweza kusimamisha kurekodi kwa kufinya STOP utaona kwenye kio TOC EDIT hii huonyesha mashine ina save track uliyo rekodi, usiitigishe mashine ama ukazima umeme ama stima kama unatumia adaptor wakati inafanya TOC EDIT kwani unaweza kuharibu minidisc.

• Kucheza minidisk finya kitufe kilichoandikwa play button na utaweza kusikia ulicho rekodi unaweza kupeleka mbele ukitumia fast-forward au kurudisha nyuma ukitumia rewind.

• Ukita kucheza tracks mbalimbali finya stop halafu finya fast forward ama rewind.

• Ukitaka kufuta track finya kitufe cha pause halafu finya play halafu finya pause tena finya fast forward ama rewid ukitafuta kile unachotaka kufuta ama track finya track mark button, sasa unaweza kufuta track moja baada ya nyengine.

• Ukitaka kufuta track zote finya kitufe kilichoandikwa STOP, halafu bonyeza EDIT na shikilia kwa sekunde mbili hivi halafu finya fast forward ama rewind huku ukiangalia display ama kioo mpaka uyaone maadishi ya ERASE baadae bonyeza PLAY/ENTER button kisha ERASE. Finya PLAY /ENTER halafu utaona maandishi EDIT kwenye display/Kioo sasa minidisk imefutika.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA