MASHINDANO YA SAFARI LAGER NYAMA CHOMA 2012 YAZINDULIWA

Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Oscar Shelukindo akiwaongoza watu wengine kula nyama choma, wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Safari Lager Nyama Choma 2012 , Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa TBL inayozalisha bia hiyo,Mamongae Mahtare, Jaji Mkuu msaidizi wa mashindano hayo, Lawrence Salvi, Mtangazaji wa TBC, Jane John
Shelukindo (kushoto) na Salvi akiendelea kuonja nyama hizo




Shelukindo akiwa amenogewa na mshikaki
Wanahabari nao hawakuwa nyuma katika kuonja nyama hiyo iliyochomwa kitaalamu
Jaji Mkuu msaidizi wa mashindano hayo, Salvi (kulia)akielezea jinsi mashindano hayo yatakavyoendeshwa. Kushoto ni Shelukindo wa TBL.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imezindua rasmi yale mashindano ya aina yake na ya kuvutia ya kuchoma nyama yajulikanayo kama “Safari Lager Nyama Choma”
Mashindano haya hushirikisha majiko ya baa mbalimbali katika umahiri wa kuchoma nyama na hatimaye zawadi hutolewa kwa washindi.
Akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya mwaka huu, meneja wa Bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo alisema madhumuni makubwa kwa bia ya Safari lager kuendesha mashindano haya ambayo yamekuwa kivutio kwa walaji wa nyama na watumiaji wa bia ni kuhakikisha tunaleta changamoto kwa majiko yanayochoma nyama, ili kuhakikisha walaji wanapata kile kilicho bora kabisa.
Watumiaji wa bia ya Safari Lager, hupendelea sana kuitumia huku wakisindikiza na nyama choma iliyoandaliwa vizuri, hivyo kupitia mashindano haya, bia ya Safari Lager inaendeleza utamaduni wa kunywa bia na kula nyama. Kufuatia ubora wa hali ya juu wa bia ya Safari lager, tunafurahi sana pale ambapo mnywaji atapata pia nyama iliyo bora ili mtumiaji aweze kuridhika zaidi.

Mashindano ya mwaka huu yatafanyika katika mikoa mitano ambayo ni; Dar Es Salaam, Kilimanjaro, Arusha,Mbeya.na Mwanza. Kuna ongezeko la mkoa wa Mwanza ambao mwaka juzi haukushiriki. Ni matarajio ya bia ya Safari Lager kuyapeleka mashindano haya katika mikoa yote siku za usoni.
Akitaja zawadi za washindi, Shelukindo alisema; baa itakayoshika nafasi ya kwanza itajinyakulia shilingi Milioni Moja, mshindi wa pili, Laki Nane, Mshindi wa Tatu laki Sita, Nafasi ya Nne; Laki Nne na nafasi ya Tano shilingi Laki Mbili. Zawadi hizi zimegawanywa kwa kila mkoa.
Utaratibu wa kupata baa zitakazoshiriki mashindano haya utaendeshwa kwa njia ya simu, ambapo wananchi watatakiwa kutuma ujumbe mfupi usemao “Safari kisha Mkoa uliopo ikifuatiwa na jina la Baa” kisha tuma kwenda namba 0763 514 514 Utapokea ujumbe kukuhakikishia kuwa kura yako imepokelewa.
Jopo la majaji litapitia kura zote na Baa ishirini kwa Dar Es Salaam na Kumi kwa mikoa mingine zitakazokuwa zimepata alama za juu zaidi ndizo zitakazopambana katika hatua ya pili ya tano bora ambapo majaji watazitembea tena na kutoa maksi kulingana na vigezo waliovyo navyo kasha baa hizo zitapambana katika eneo la wazi ambapo mandhari ya kula nyama na kunywa bia itakuwa imeandaliwa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.