KWA HERI MPIGANAJI SAMSON MBEGA

Baadhi ya waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe, Marehemu Samson Mbega katika Kanisa la KKKT Usharika wa Wailes, Temeke, Dar es Salaam, muda mfupi kabla ya kusafirishwa kwenda kwao Kisarawe, mkoani Pwani kwa mazishi. Marehemu Mbega ameacha watoto watatu.
Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Amir  Mhando, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu, Samson Mbega.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Perfect Solutions, Evans Aveva akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Samsopn Mbega, aliyewahi kufanyia kazi gazeti la Ngurumo za Simba lililokuwa linamilikiwa na kampuni hiyo.
Wanafunzi wanaosoma na mtoto wa marehemu Samason, Noah Samson wakitoa heshima za mwisho
Mhariri Mtendaji wa gazeti la Nipashe, Jese Kwayu (kushoto), Mwandishi wa habari wa gazeti hilo, Bawazir (kulia) wakiwa na huzuni wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marahemu Samson
Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe, marehemu Samson Mbega, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Wailes,Temeke, Dar es Salaam, baada ya kuombewa kabla ya kusafirishwa kwenda kwao Kisarawe kwa mazishi. (PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA) 
Mwili ukiingizwa kwenye gari maalum tayari kwa safari ya kwenda Kisarawe
Baadhi ya waombolezaji wakitoka kanisani baada ya kutoa heshima za mwisho
Mama wa marehemu Samson, Bibi Catherine Mbega akifarijiwa na ndugu
Mwandani wa marehemu Samson akilia kwa uchungu wakati wa kuaga
Mmoja wa watoto wa marehemu Samson, Noah akiwa na majonzi baada ya kutoa heshima za mwisho
                                                                   Baadhi ya waombolezaji

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO

TOFAUTI YA WATU WA DAR NA WA MKOANI NI HUU

IBENGE: YANGA SC WATAFUZU HATUA YA ROBO FAINALI.

NILIYOYABAINI KATIKA TRENI YA SGR DAR ,MORO HADI DODOMA … KADOGOSA REKEBISHENI MAMBO HAYA MTANIKUMBUKA