NHIF ILIVYOKUTANA NA WADAU ARUSHA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Arusha.
Naibu Mkurugenzi wa NHIF, Hamis Mdee akitoa maelezo ya utangulizi kwa mgeni rasmi.

Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji wa NHIF, Bw. Rutazaa akiwasilisha mada ya utekelezaji ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuanzia mwaka 2001.
Wadau wa mkutano huo wakifuatilia mada.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akifurahia jambo na
Mjumbe wa Bodi ya NHIF, Mama Mwanaidi Mtanda.

Wadau wakiwa makini na ufuatiliaji wa mada.
Wakuu wakiagana baada ya ufunguzi wa mkutano huo.
 Meneja wa Kanda ya Kaskazini Magharibi, Bi. Alesia akiwasilisha
mada ya utekelezaji wa Mkoa wa Arusha katika Mifuko ya NHIF/CHF
Madaktari wakiendelea na uzoezi la upimaji kwa wadau waliohudhuria mkutano huo ikiwa ni moja ya shughuli zinazoambatana na siku za wadau.

RC: Uhakika wa afya bora ni kujiunga na NHIF/CHF
Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo amesema uhakika wa afya bora kwa wananchi mkoani huo utapatikana endapo viongozi watahamasisha ipasavyo wananchi kujiunga na Mfuko ya Taifa ya Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF).
Kutokana na hali hiyo amewataka wadaua wote kuweka mikakati na mbinu za kuhakikisha suala la wananachi kujinga kwenye utaratibu wa Bima hususan Mfuko wa Afya ya Jamii linatekelezwa.
Mulongo aliyasema hayo jijini hapa jana wakati wa uzinduzi wa Mkutano wa Wadau ambao pamoja na mambo mbalimbali utaweka maazimio ya kuhakikisha wananchi mkoani humo wanajiunga na utaratibu wa Bima ya Afya lakini pia kuboresha huduma za matibabu katika vituo vya kutolea huduma.
"Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeonesha dhamira ya kusaidia juhudi za mkoa katika kufanikisha suala hili, hivyo ni vyema na sisi tukaongeza jitihada za kuhamasisha wananchi kujiunga na CHF," alisema Mulongo na kuongeza kuwa
"Uendelevu wa Mifuko hii unategemea sana ushirikiano wa viongozi tuliopo hapa, Kiongozi mmoja akipuuza majukumu yake ya msingi katika suala la afya itasababisha ugumu mkubwa katika azma ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma za matibabu zinazostahili na kwa urahisi," alisema.
Ili kutekeleza hilo, aliziagiza Halmashauri za Mkoa huo kuhakikisha zinajipanga kikamilifu na kubuni mikakati itakayowezesha watu wengi kujiunga na Mifuko hiyo ya afya ikiwa ni pamoja na kutoa elimu na kuhakikisha ubora wa huduma na hasa suala la upatikanaji wa dawa.
"Wote wanaohujumu au kutowajibika ipasavyo katika kuleta mafanikio ya suala hili wawajibishwe kwani bila afya bora hakuna shuguli yoyote ya kiuchumi inayoweza kufanyika hivyo suala la afya ni la msingi kwa ustawi wa wananchi wetu," alisema Mulongo.
Akizungumzia watoa huduma, aliwataka kufanya kazi kwa kuzingatia maadili yao lakini pia kuwathamini wanachama wa Mifuko hiyo na kuachana na dhana ya kuwaona hawana umuhimu wowote kwani mifuko hiyo inaingiza mapato makubwa yanayoweza kuboresha huduma za matibabu na hasa kupunguza tatizo la ukosefu wa dawa na vifaa tiba.
Kutokana na hayo, Mkuu huyo wa Mkoa aliahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya katika mkoa huo ili uweze kufanikisha azma yake ya kuwafikia asilimia 30 ya wananchi wote ifikapo mwaka 2015.
Naye Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHIF, Mwanaidi Mtanda, alisema kuwa uamuzi wa kuwa na siku ya wadau ulilenga kuimarisha ushiriki wa wadau wa ngazi zote, kupata maoni zaidi na kupata suluhisho la changamoto zinazoukabili Mfuko na kuwa na uwajibikaji wa pamoja kwa mambo yanayoafikiwa na kuazimiwa ili hatimaye huduma za afya ziwe bora zaidi kwa wanachama.
Aidha Mtanda alitumia fursa hiyo kuhamasisha fursa ya mikopo ya vifaa tiba inayotolewa na Mfuko huo ili vituo viwe na uhakika wa kutoa matibabu bora zaidi.
"Niwaombe tu viongozi wote hususan wa kisiasa tusaidieni kuhamasisha wananchi kupitia majukwaa yenu ya kisiasa ili dhana ya bima ieleweke vizuri kwani lengo letu ni afya bora kwa wote." alisema Mtanda.
Kwa upande wake Naibu Murugenzi wa NHIF, Hamis Mdee alielezea mambo mbalimbali yanayofanywa na Mfuko kuhakikisha huduma kwa wanachama zinaboreshwa lakini pia akawataka wadau hao kuwa wawazi ili hatimaye majibu ya changamoto wanazokumbana nazo yapatikane.
Ciooo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.