TBL YASAIDIA UCHIMBAJI VISIMA VYA MAJI MOROGORO

Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo  (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 24.9 Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, Dk. Ntobi Mwakibete za kusaidia kuchimba kisima cha maji.  Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo  (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 26.7, Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amiri Nondo kwa ajili ya mradi wa maji kwa shule 12 za sekondari za manispaa hiyo.Kulia ni Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Uchimbaji Visima vya Maji ya Jae-Hi-Tech Dry Cleaning, Maximillian Makota na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Jovis Simbeyi. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.

Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amiri Nondo akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 26.7, Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Uchimbaji Visima vya Maji ya Jae-Hi-Tech Dry Cleaning, Maximillian Makota zilizotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa ajili ya uchimbaji wa visima vya maji mkoani humo. Kulia ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.
Ofisa Ustawi Jamii Sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro, Tabitha Majiku  (kulia) akitoa neneo la shukrani baada ya kupokea msaada wa fedha za kusaidia miradi ya maji mkoani humo kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro. Kutoka kushoto ni  Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo  na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, Dk. Ntobi Mwakibete (wa pili kulia).

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Soma Taarifa ya UTEUZI:Rais Jakaya Kikwete amemteua Dkt. Ben E. Moshi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya PUMA Energy (zamani ilijulikana kama BP Ltd)

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MAAFISA JENERALI WASTAAFU 17 WA JWTZ WAAGWA.

PICHA YA RAIS ILIYOBAMBA WIKI HII

JUA AINA NNE ZA KABILA LA WASUKUMA

18 WAPITISHWA KUGOMBEA UONGOZI YANGA

BINTI WA KITANZANIA GLORIA MAJULE ASHINDA TUZO YA UANDISHI BORA WA FILAMU YA MALARIA MAREKANI ‎

DK MAGUFULI ATANGAZA KIAMA CHA MAJAMBAZI, WEZI NA MAFISADI KATIKA MIKUTANO YA KAMPENI SUMBAWANGA,TUNDUMA, ILEJE NA MBOZI