MECHI YA SIMBA NA YANGA YAINGIZA SH. MIL. 260

Mashabiki wa Simba wakishangilia ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Yanga

KIASI cha Sh. Milioni 260 kimepatikana kutokana na mechi ya funga dimba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baina ya watani wa jadi SImba na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kutokana na idadi ya watu 41,733 walioingia.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo, ameiambia BIN ZUBEIRY machana huu kwamba, watazamaji 4 viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 10,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 VIP C, sh. 30,000 VIP B na sh. 40,000 VIP A. Alisema watazamaji 36,980 walinunua tiketi za sh. 5,000 wakati 203 walikata za sh. 40,000 na jumla ya Sh. 260,910,000 zilipatikana.
Alisema Kila klabu ilipata Sh. 62,646,395.85, wakati asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni Sh. 39,799,830.51 na TFF ilijimegea Sh. 19,908,361.95.
Alisema gharama za mechi kabla ya mgawo ni nauli ya ndani ya waamuzi na kamishna sh. 20,000, posho ya kujikimu kwa kamishna sh. 40,000 na mwamuzi wa akiba sh. 30,000, gharama za tiketi sh. 8,539,950, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, ulinzi na usafi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.
Alisema mgawo wa uwanja ni sh. 19,908,361.95, gharama za mechi sh. 19,908,361.95, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 9,954,180.97, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 1,990,836.19 na Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA) kilimegewa Sh. 10,467,324.78.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.