Bajeti ya Magufuli Sh1 trilioni

KAMATI ya Bunge ya Miundombinu imeipitisha bajeti ya Wizara ya Miundombinu, ambayo ni Sh1,023,033,626,000.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Peter Serukamba, alisema kipaumbele cha wizara katika bajeti hiyo ni kuhakikisha barabara zote nchini zinaunganishwa kwa kiwango cha lami.


Juzi, Waziri wa Fedha na Uchumi, William Mgimwa, alisema bajeti ya Serikali kwa mwaka 2012/13 inatarajiwa kuwa Sh15 trilioni katika vipaumbele saba. Bajeti inayomalizika ilikuwa Sh13.5 trilioni.
Serukamba alisema katika miradi ya maendeleo, fedha za ndani ni Sh296,896,892,000 na fedha za nje ni Sh397,051,380,000 na kwamba, jumla ni Sh693,948,272,000.

“Mishahara ya wizara na taasisi ni Sh21,340,508,000, mfuko wa barabara Sh300,764,800,000, matumizi mengine ni Sh6,980,046,000 na jumla yake ni Sh329,085,354,000,” alisema Serukamba.
Alisema bajeti hiyo imepita kwa urahisi kwa sababu fedha nyingi zimepelekwa katika miradi ya maendeleo.

“Serikali imeshapata fedha kwa ajili ya kulipa madeni yote ya wizara ambayo mpaka mwishoni mwa Juni mwaka huu yatakuwa yamelipwa. Ila tumewataka kuhakikisha msongamano wa magari Mwanza, Dar es Salaam na Arusha unakwishwa,” alisema Serukamba.


Alisema barabara zote za Dar es Salaam zimechukuliwa na Wakala wa Barabara (Tanroads) na zitajengwa kwa kiwango cha lami.
Vipaumbele katika bajeti hiyo ni miundombinu ambayo ina vipengele vinne; umeme, usafirishaji na uchukuzi, mawasiliano na maji salama.

Vipaumbele vingine ni kilimo, viwanda, rasilimali watu na huduma za jamii, utalii, biashara za ndani na n je na huduma za fedha.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO

CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO

NILIYOYABAINI KATIKA TRENI YA SGR DAR ,MORO HADI DODOMA … KADOGOSA REKEBISHENI MAMBO HAYA MTANIKUMBUKA