MPIGANIA HAKI ZA MADAKTARI STEPHENE ULIMBOKA YU HOI BAADA YA KUPIGWA NA WATU WASIOJULIKANA. MASHUSHU WAWILI WAPIGWA NA MADAKTARI, WAPIGAPICHA WAPATA KIBANO
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari inayoongoza mgomo wa madaktari, Stephene Ulimboka akiwa hoi baada ya kupigwa na watu wasiojulikana na kutupwa eneo la Mwabepande, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Inadaiwa aliokotwa vichakani na watu wasiojulikana, na baadaye asubuhi hii kukimbizwa Hospitali ya Taifa ya Mihimbili, Dar es Salaam, ambako anaendelea kupata tiba.
Ulimboka alipofikishwa Muhimbili kwa Ambulance ya AAR, madaktari na wauguzi walangua vilio na kughalaghala chini.
Askari wa Usalama wa Taifa walizagaa eneo la Muhimbili na kuwazuia waandishi wa habari na wapigapicha ili wasipate tukio hilo.
Karibu kila mpiga picha aliwekewa ulinzi wa mashushu, ambao kazi yao ilikuwa kuwazuia kufanya kazi yao ya kupiga picha. Baadhi ya wapiga picha akiwemo Kamnada wa Mwaikenda, walionja adha hiyo.
Pia katika sakata hilo, madaktari wenye hasira, waliwapatia kipigo kikubwa mashushu wawili waliowashitukia wakifuatilia kuwasili kwa mwili wa Ulimboka Muhimbili..
akiuliza swali wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipozungumza na madaktari na wauguzi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam, Februari 9,2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Comments