NDOTO ZA MAXIMO KUTUA YANGA KITENDAWILI



Ndoto za Klabu ya Yanga yenye Maskani yake mtaa wa Jangwani jijini Dar es Salaam za kumtwaa kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Tabnzania “Taifa Stars” Mbrazili, Marcio Maximo huenda zikayeyuka kufuatia kocha huyo kuwa na mkataba Nchini Brazili.

Katika salamu zake kwa wana Yanga na watanzania kwa Ujumla Maximo amesema sio rahisi rahisi tu yeye kuja kuifundisha Yanga kwani bado wapo katika mazungumzo.

“Ni kweli nimepokea Mkataba kutoka Yanga, lakini bado tupo katika majadiliano kwasababu bado nina mkataba hapa, hivyo sio rahisi kuchukua maamuzi ya haraka”, alisema Maximo.

Aidha Maximo amesema anajisikia furaha sana na maamuzi ya Clabu ya Yanga kumhitaji yeye kukinoa kikosi hicho, lakini mbali na Yanga kumhitaji anasema pia timu kadhaa za afrika zimemhitaji zikiwepo mbili za taifa.

Amezitaja timu zinazomhitaji ni pamoja na St George ya Ethiopia pamoja na timu za taifa za Rwanda na Zimbabwe.

Aidha Kocha huyo aliyeleta ari ya watanzania kuipenda timu yao ya Taifa na soka la nyumbani kwa kauli zake za matumini “ Pamoja Tutashinda” amesema anaendelea kuifikiria Yanga maana uongozi umeonesgha nia ya kutaka kuiboresha timu.

Mapema wiki hii, Viongozi wa Yanga walidai kuwa Kocha huyo Mbrazil angewasili nchini jana tayari kwa kuinona timu hiyo iliyo poteza ubingwa kwa kichapo cha magoli 5-0 kutoka kwa mahasimu wao wakubwa Yanga na Kichapo kutoka kwa wapinzani wao wa karibu Azam kilichopelekea Yanga kuambulia nafasi ya 3 na kufungiwa kwa baadhi ya wachezaji wake. 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AINA 4 ZA WANAWAKE WASIOWEZA KUDUMISHA NDOA.

MVUA KUBWA KUNYESHA MIKOA 20

MIKOA 10 YENYE KIPATO KIKUBWA ZAIDI KWA MTU MMOJA MMOJA

BODABODA ALIPWA PIKIPIKI BAADA KUSAFIRI KWA BODA KWA SAA 10 MBEYA HADI DAR

CONFIRMED HAWA NDIO WACHEZAJI WETU 12 WA KIGENI 🦾