Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani maarufu kwa jina la Profesa Maji Marefu (pichani), leo amesema bungeni kuwa kipigo alichopata Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka, kinastahili ili naye apate machungu wanayopata waginjwa wengine mahospitalini.
Profesa Maji Marefu aliitoa kauli hiyo wakati akichangia hoja katika bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, bungeni Dodoma.
Kauli hiyo ilisababisha tafrani kidogo bungeni na kumfanya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuingilia kati kumzuia Maji Marefu asiendelee kutoa kauli hiyo kwani jambo la madaktari bado liko mahakamani.

Comments