SINA UGOMVI NA WAZIRI, ANENA KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Seth Kamuhanda (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana,  kukanusha habari zilizoandikwa kwenye vyombo habari kwamba haelewani na waziri wake. Kushoto ni Gasper Mwembezi ambaye ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa wizara hiyo. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

WIZARA ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imekanusha taarifa kuwa kunamsuguano kati ya Waziri na Katibu Mkuu katika Wizara hiyo.
Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Seth Kamuhanda wakati alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari  jijini Dar es Salaam leo .
Alisema taarifa hizo zilizoandikwa na Jukwaa la wa Hariri Tanzania (TEF),  kwenye vyombo vya habari kuwa hazina ukweli wowote kwani viongozi hao wamekuwa na  ushirikiano mzuri  kati kazi hivyo si rahisi kutokea migongano kama ilivyodaiwa.
Kamuhanda alisema nawaomba wanahabari mkitoka hapa muwafikishiye taarifa hizi wananchi  kuwa katika Wizara hiyo hakuna migongano na wahakikishia kuwa haitatokea kwa kuwa hakuna tofauti yeyote kati yao.
"Unajua hali kama hiyo ya mimi kugongana na waziri kwa kuwa kila mmoja wetu amekuwa akifanya kazi yake kwa uadilifu mkubwa hivyo basi haitatokea hata siku moja kutokea tofauti.
Akizungumzia ni kwa nini walishindwa kufika siku ya kufungua na kufunga mkutano huo alisema taarifa waliyopaswa kujibu na Baraza la Wahariri kutokana na ukweli kwamba waliwafikishia taarifa ya kutofika.
Kamuhanda alisema wakati walipopata mwaliko kipindi hicho Wizara ilikuwa katika maandalizi kuhusu kamati za Bunge jambo ambalo liliwafanya washindwe kuhuria kikao hicho ambapo walifikisha taarifa kwa Watendaji wa jukwaaa.
"Kwa kweli nilishangaa niliposoma hiyo taarifa kwa kuwa tulikwisha zungumza kuhusu kutohudhuria kwetu katika kikao hicho.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DK MAGUFULI ATANGAZA KIAMA CHA MAJAMBAZI, WEZI NA MAFISADI KATIKA MIKUTANO YA KAMPENI SUMBAWANGA,TUNDUMA, ILEJE NA MBOZI

VIONGOZI BORA BARANI AFRIKA KWA SASA.

UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MSALATO DODOMA KUANZA KUTUMIKA SEPTEMBA 2026

BALOZI WA CHINA KUPITIA DKT. MAJULE APELEKA NEEMA KWA WANAWAKE DODOMA

SERIKALI YAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO NA DIT KUIMARISHA USIMAMIZI WA MAAFA

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA