TBL YATOA VIFAA VYA USAFI VYA SH. MIL 12 MANISPAA YA ILALA,YASHIRIKI USAFI WA MAZINGIRA


Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, msaada wa vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh. milioni 12 kwa ajili ya Manispaa ya Ilala, wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Mazingira Duniani, Dar es Salaam jana.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, akiendesha moja kati ya matolori yaliyotolewa msaada na TBL kwa Manispaa ya Ilala. Kulia ni Steve Kilindo wa TB

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mushi (kushoto) na Steve Kilindo wa TBL wakifagia ikiwa ni ishara ya kuzindua rfasmi maadhimisho hayo juzi karibu na Soko la Mchikichini, Ilala, Dar es Salaam.

Mfanyakazi wa TBL, akimvisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi kifaa cha kuzuia vumbi kabla ya kuanza kufanya usafi.



 Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakiungana na watumishi wa Manispaa ya Ilala kufanya usafi wa mazingira katika makutano Barabara ya Uhuru na Mtaa wa Muheza, Karikaoo, Dar es Salaam jana. TBL ilitoa msaada wa vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh. mil. 12 kwa Manispaa ya Ilala wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Mazingira, Dar es Salaam jana.
 Watumishi wa Manispaa ya Ilala na Wafanyakazi wa TBL, wakifanya usafi kwenye Mtaa wa Muheza, Kariakoo.
 Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa TBL, Emma Oriyo (katikati), akizoa taka wakati wa kampeni hiyo ya usafi wa mazingira
Mtaa wa Muheza, Kariakoo ukipendeza baada ya kufanyiwa usafi.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA