BALOZI ZAADHIMISHA MIAKA 94 YA MANDELA KWA KUKARABATI SHULE YA TANDALE


Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Afrika Kusini nchini wakiwa wamekusanyika katika shule ya Msingi Tandale jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyakazi za kujitolea kwa dakika 67 ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 18 mwezi Julai.
Balozi wa Uganda nchini Tanzania Mh. Ibrahim Mukiibi akiwasili kushiriki zoezi hilo.
Mabalozi wa Afrika Kusini Mh. Henry Chiliza (kushoto) na Mh. Ibrahim Mukiibi wa Uganda wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania wakisalimiana baada ya kukutana katika zoezi la kujitolea kufanya kazi za kijamii katika shule ya msingi Tandale ya jijini Dar es Salaam. Kulia ni Joymrey Von de Merwe.
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) Bi. Stella Vuzo akitoa mwongozo wa namna ya kutekeleza zoezi hilo ambalo limeonyesha mafanikio makubwa baada ya kuweza kukarabati madawati yalioharibika, kupiga rangi Ubao za kuandikia madarasani na kufanya usafi katika mazingira ya shule hiyo.
Bi. Stella Vuzo amesema katika kuadhimisha siku kama hii mwaka jana Umoja wa Mataifa ulitoa huduma za Kibinadamu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa wa Saratani na mwaka huu wameonelea ni vyema kuungana na wanafunzi wa shule ya msingi Tandale kwa kuonyesha wanajali na kutoa huduma kama hizo katika shule hiyo chini ya kauli mbiu ya mzee Nelson Mandela "Inspire Change Within Your Self".
Wafanyakazi wa UN na Ubalozi wa Afrika Kusini wakishirikiana kubeba madawati kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati.
Pichani Juu na Chini ni Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Tandale jijini Dar Hamisi Kubiga (kushoto) sambamba na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania Mh. Henry Chiliza wakihakikisha ukarabati wa madawati unakwenda sawa.
Balozi wa Uganda nchini Mh. Ibrahim Mukiibi akifanya usafi katika moja ya madarasa ya Shule hiyo.
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) Bi. Stella Vuzo akitumia muda wake wa dakika 67 kusafisha maeneo ya shule ya msingi Tandale ya jijini Dar.
Mfanyakazi wa Ubalozi wa Afrika Kusini nchini Masoud Ramadhani (kushoto) akichanganya dawa kwa ajili ya kusafisha vyoo vya shule ya msingi Tandale katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela.
Wanafunzi na wafanyakazi wa UN na Ubalozi wa Afrika Kusini wakisaidiana kuzoa taka kuhakikisha shule ya msingi Tandale inakuwa safi.
Wanafunzi wakionyesha ushirikiano katika kuadhimisha Nelson Mandela International Day.
Pichani Juu na Chini Wafanyakazi wa UN na Ubalozi wa Afrika Kusini wakipiga rangi Ubao wa Kufundishia katika shule ya msingi Tandale jijini Dar es Salaam.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA