Mchezaji Nadir Haroub (kulia) wa Yanga akipiga mpira huku Jaku Juma wa Mafunzo ya Zanzibar akiruka katika mechi ya robo fainali ya kuwania Kombe la Kagame, jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji wa Mafinzo ya Zanzibar, wakishangilia bao la kuongoza dhidi ya Yanga
Kelvin Yondani wa Yanga akiruka kuokoa hatari dhidi ya timu ya Mafunzo
Aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Kongwa, Job Yustino Ndugai amefariki Dunia leo August 06,2025 akiwa anaendelea kupatiwa matibabu Hospitalini baada ya kuugua ghafla. Kwa mujibu wa taarifa ya Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson aliyoitoa imesema: “Kwa masikitiko makubwa, naomba kutoa taarifa ya kifo cha kiongozi wetu, mwanasiasa mkongwe na Spika mstaafu wa Bunge, Job Ndugai kilichotokea leo jijini Dodoma. “Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na wananchi wa Jimbo la Kongwa, Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu.” Dk Tulia amesema Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na kamati ya mazishi pamoja na familia ya marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa. Ndugai amekuwa Spika wa Bunge tangu November 17, 2015 hadi Januari 06, 2022 alipojiuzulu na kuendelea kuwa Mbunge wa Kongwa nafasi ambayo ameendelea kuitetea kwa kuchukua fomu tena mwaka huu ambapo ameshinda kwenye kura za maoni.
# KWENYE #MAISHA #YAKO 1. Weka Mipaka ya Heshima (Set Boundaries): Sio kila mtu wa kumsaidia, sio kila mtu anastahili huruma yako. Tofautisha kati ya utu na kupuuzwa. 2. Jifunze Kusema “Hapana”: Ukitaka heshima, usiwe mtu wa ndiyo kwa kila jambo. Ukitumia nguvu zako hovyo, utamaliza heshima yako. 3. Jithamini Kabla Hujathamini Wengine: Usijitoe sadaka kwa watu ambao hata hawakuulizi unaendeleaje. Jiamini, jipende, jikubali. 4. Chagua Mpenzi Mwenye Moyo wa Kuthamini, Sio Kuokoa: Kama mwanamke ana majeraha ya zamani, hakikisha anajiponya mwenyewe. Usijaribu kuwa "daktari wa moyo wake" ukitegemea atakupenda zaidi. 5. Tafuta Misingi ya Maisha Yenye Malengo (Purposeful Living): Usijifungie kwenye kazi au mapenzi tu. Kuwa na maisha yenye dira: ndoto zako, afya yako, marafiki wa kweli. 6. Kua Kifedha na Kisaikolojia (Grow Financially & Emotionally): Jifunze uwekezaji, epuka utegemezi, weka akiba. Pia jifunze kujieleza, kusamehe, kujijenga kihisia. 7. Usikubali Uonevu Kazini a...
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Alliance for Democratic Change (ADC), Wilson Elias Mulumbe (katikati) aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Shoka Khamis Juma (kushoto) katika tukio lililofanyika Agosti 14, 2025 Njedengwa jijini Dodoma. Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kuchukua fomu, Mgombea pendekezwa wa Urais wa chama hicho, Mulumbe amesema kuwa chama chake kikishinda atahakikisha anafuta madeni yote wanayodaiwa wanafunzi na Bodi ya Mikopo, itakuwa elimu bure, afya bure na wateja wataunganishiwa umeme bure. Vyama vingine vilivyochukua fumu jana Agosti 13, 2025 ni; Chama cha Democratic Party (DP), Abdul Juma Mluya (Urais) aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Masoud Abrahman Khatib na Cha...
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Dk Samwel Shelukindo imeeleza kwamba, imepokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu, Kiongozi Balozi Dk Moses Kusiluka ikitaarifu kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa mamlaka aliyo nayo chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametengua uteuzi wa Humphrey Polepole, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kumuondolea hadhi ya ubalozi. Aidha, Rais Samia kwa mamlaka aliyonayo chini ya sheria ya utumishi wa umma amemuachisha kazi Polepole kwa manufaa ya umma.
Tanzania yaitaka Miss World 2027! Dkt. Samia Afanya Mazungumzo Ndoto ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa ya urembo, Miss World 2027, imechanua baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufanya mazungumzo muhimu na uongozi wa Kampuni ya Miss World Limited. Kikao hicho cha kihistoria kilifanyika Julai 20, 2025, huko Kizimkazi, Zanzibar. Uongozi wa Miss World Limited uliongozwa na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wake, Bi. Julia Evelyn Morley, akiambatana na mshindi wa taji la Miss World 2025, Bi. Opal Suchata Chuangsri kutoka Thailand, pamoja na Miss World Africa, Bi. Hasset Dereje Admassu kutoka Ethiopia. Mazungumzo hayo, ambayo pia yalihudhuriwa na viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, pamoja na viongozi wa Maliasili na Utalii, yalilenga kujadili namna Tanzania inavyoweza kuandaa kwa mafanikio makubwa mashindano hayo makubwa ya kimataifa. Mazungumzo haya kati ya Rais Dkt. Samia na uongozi wa Miss World yana...
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kenani Kihongosi akisalimiana na waandishi wa habari baada ya kumaliza kuzungumza nao katika Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dodoma Julai 20, 2025, kuhusu mafanikio ya mkoa huo katika miaka minne ya Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kenani Kihongosi akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dodoma Julai 20, 2025, kuhusu mafanikio ya mkoa huo katika miaka minne ya Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan. Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO, Rodney Kihongosi akitoa neno la kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kihongosi kuzungumza na waandishi wa habari. Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo. MAFANIKIO YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA KATIKA MKOA WA ARUSHA Awali ya yote nichukue nafasi hii kumshuru sana Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema, kwa kutujalia kukutana hapa siku ya leo tukiwa wazima na afya njema, huku tu...
Comments