HAMAD RASHID ATAKA CUF IJITOE SERIKALI YA MSETO

MBUNGE wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), amelaani matumizi ya nguvu za Jeshi la Polisi wakati wa chaguzi mbalimbali huku akikishauri chama chake kujiondoa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa baina yao na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na kutowasaidia wananchi.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu, Hamad alisema kuwa ameshangazwa na nguvu kubwa ya Jeshi la Polisi iliyotumika katika uchaguzi mdogo wa Bububu uliomalizika hivi karibuni na hivyo kusababisha kujeruhi wananchi bila sababu.

Alisema CUF iliingia katika serikali ya mseto kwa lengo la kuweka uhuru na haki lakini wameshindwa kufikia azima hiyo na kwamba ikiwa muafaka huo ni kwa maslahi ya watu wachache basi wajitoe.

“Mimi nashangaa sana hayo mazungumzo sijui yalikuwa ya nini na ‘ndoa’ ilikuwa ya nini kama ilikuwa ni kwa masilahi ya watu wachache huku wananchi hawanufaiki nayo, wanapigwa risasi, basi CUF wajiondoe kama si kwa masilahi ya wananchi wote,” alisema Hamad.

Hata hivyo, Hamad alisema Serikali ya Zanzibar inaundwa na vyama viwili, hivyo ni dhahiri kwamba CCM na CUF ndio wametumia nguvu katika kuvikandamiza na kuhujumu vyama vidogo vya siasa ambavyo havikuwa na serikali.

Katika uchaguzi huo wa Jumapili ambao CCM iliibuka kidedea ikifuatiwa na CUF na Chama kipya cha ADC, vurugu kubwa zilizuka huku matokeo hayo yakipingwa vikali.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.