KIPINDI CHA LADY JAYDEE KUANZISHWA TELEVISHENI YA EATV

Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura 'Lady Jaydee' (kulia), akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Nyumbani Lounge, Oysterbay, Dar es Salaam leo, kuhusu maandalizi ya uzinduzi wa kipindi chake kipya cha Lady Jaydee Diary, kitakachokuwa kikirushwa hewani na kituo cha Televisheni cha East African (EATV), maarufu kama Channel 5 kila Jumapili saa 3:00 usiku. Kushoto ni Mkuu wa vipindi EATV, Lydia Igarabuza. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)



MWANAMUZIKI mkongwe nchini, Lady Jadee ameanzisha kipindi cha TV kiitwacho Diary Ya Lady Jaydee, kitakachokuwa kikirushwa hewani na kituo cha East African TV, maarufu kama Channel 5 kila Jumapili saa 3:00 usiku.
 
Kama msanii, Lady Jaydee amefanikiwa na kutambulika katika kiwanda cha muziki ndani na nje ya nchi, huku akitunukiwa tunzo nyingi zaidi akiwa albamu zake tano. Pamoja na kuwa anaendelea na fani yake ya muziki, Lady Jaydee ameamua kuwafikia na kuwaburudisha wapenzi wa kazi zake kwa njia nyingine.
Lady Jaydee sasa anaanza sura mpya ya burudani kwa kuleta kipindi cha TV kiitwacho DIARY YA LADY JAYDEE, ambacho kutaonekana katika kituo cha TV cha EATV
 
Diary Ya Lady Jaydee itaonesha maisha na hadithi za kweli za Lady Jaydee kwa lengo la kuburudisha kwa kuonyesha mambo yate mazuri anayopitia au kuyaona Lady Jaydee kuelimisha kwa kushiriki mambo ya kijamii, kutia moyo wengine wafuate ndoto zao kwa uadilifu, kuongeza kipato kama msanii kwa kutangaza biashara mbalimbali na hatimae kudumisha ajira binafsi kwa njia ya sanaa.
 
Lady Jaydee anatoa shukrani kwa mashabiki kwa kuendelea kumpokea, jambo ambalo linampa nguvu zaidi ya kufanya kaza.
 
Pia anashukuru sana vyombo vya habari na zaidi anawashukuru EATV na washirika wake kwa kumpa nafasi ya kurusha kipndi chake kipya Diary Ya Lady Jaydee. EATV imekuwa mchango wa aina yake katika kuwakuza wasanii Tanzania.
 
Lady Jaydee anatoa wito kwa vyombo vya habari kuendelea kushirikiana na naye kwa kila namna, ili kukuza na kuendeleza kipaji chake na sanaa ya muziki wa Tanzania kwa ujumla wake.
 
Zaidi anatoa wito kwa makampuni kishiriki na kuungana nae ili waweze kumpa nguvu msanii, kutangaza biashara zao na kushawishi ajira katika fani ya muziki.
Na mwisho Lady Jaydee anawaribisha wote kusikiliza CDs zake au kuburidika na kundi lake la Machozi Band au kupata chakula ktk mgahawa wake wa kisasa Nyumbani Lounge au ukiwa umepumzika nyumbani utazame kipindi chake Diary Ya Lady Jaydee ktk EATV.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*