MWENDESHA mkokoteni
amekufa na na watu wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kupigwa risasi
katika vurugu kubwa zilizozuka kati ya askari mgambo wa Jiji la Mwanza na wafanyabiashara ndogo ndogo
(Machinga) Jijini Mwanza leo.
Mapambano hayo yalianza majira ya saa 4:00 ausubuhi
na kusababisha maduka kufungwa pamoja na biashara mbalimbali
kutofanyika.
Tukio la kuuawa kwa mwendesha mkokoteni huyokatika soko kuu la Jiji la Mwanza, lilitokea baada ya askari
mgambo kuwafyatulia risasi machinga waliokuwa wakipambanan kuzuia mgambo hao
wasichukue mali zao .
Mgambo hao walifika eneo hilo la stendi kuu ya
zamani mabasi ya Tanganyika basi kisha kuzoa mali za wafanyaibishara hao kwa
madai kuwa wanafanya shughuli hizo kinyume cah sheria katika ameneo
yasiyoruhusiwa an halmashauri ya jiji la Mwanza.
Kutokana hali machinga hao walipinga bidhaa zao
walizopanga chini (mali) kuchukuliwa na mgambo hao
wa jiji ndipo mmoja wao aliyekuiwa na bunduki aina ya short gun akawafyatulia
risasi ambazo zilimpiga kuli huyo upande wa kushoto na kufariki
dunia papo hapo.
Mbali nakuli huyo derebva wa gari moja aina ya
canter naye alijeruhiwa sikio la upande wa kushoto na machinga mmoja kujeruhiwa
mkono wa kushoto kwenye kiwiko.
Kaimu kamnda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Ofisa
Mnadhimu (SO) SSP Lilian Matola , alitihibitisha kutokea kwa
vurugu hizo ambazo zilisababisha kifo bna majeruhi na kwamba jeshi hilo lilingia
mtaani kutuliza ghasia hizo ambazo zilidumu kwa saa nne.
Alisema askari mgambo wa jiji wanaotuhumiwa
kusababisha kifo na majeruhi hao wanashikiliwa na jeshi hilo kwa ajili ya
uchunguzi wa tukio hilo.
Kwa mujibu wa SSP Matola , mgambo hao wa jiji
walitumia risasi hizo za moto kwa nia ya kujihami na kundi la wafanyabiashara
hao ambao walikuwa wakiwashambulia kwa mawe.
Alisema majeruhi wamelazwa katika
hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC ) ya jijini hapa, huku mwili wa marehemu huyo
ukihifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali hiyo.
Aidha Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la
Mwanza, Stanslaus Mabula, aakizungumza na wandishi wa habati kwenye ukumbi wa
jiji jana jioni alisema hakukuwa na opereshani maalumu ya kuwaondo
machinga katika meneo hao bali shughuli za kawaida za halmashauri hiyo
kuhakikisha jiji liakuiwa safi.
Alisema kuwa kilichotokea ni kutokana na mgongano
wa mawazo kati ya mgambo na machinga hali iliyosababisha askari
hao wa jiji kutumia risasi za moto,hivyo akaomba radhi kwa tukio hilo na kutoia
pole kwa ndugu na familia za marehemu pamoja na ndugu wa majeruhi na majeruhi
wenyewe.
Meya huyo alisema vurugu hizo hazihusiani na
chama chochote cha siasa bali ni tukio la bahati mbaya, hivyo
uongozi wa jijini unasikitishwa mno na tukio hilo.
Alisema watuhumiwa wa tukio hilo wanashikiliwa na
jeshi la polisiu kwa ajili ya kuchunguza kama walitumia silaha vibaya.
Hata hivyo Mabula alisema kuwa pamoja na jiji
kuwa sheria ndogo ndogo bado haliwezi kuwaondoa machinga katika
maeneo ya katikati ya jiji kwa kuwa linawatambua kutokana na kazi yao ya
ujasiriamali inayowapa kipato.
leo kutwa nzima ukiondoa soko kuu biashara
mbalimbali zikiwemo za maduka na aina zingine zilishindikana kufanyika kutokana
na vurugu hizo pamoja na jeshi la polisi kutumika kuwatawanya kwa amani machinga
hao.
Vurugu kama hizo zimewahi kutokea mara kadhaa na
kusababisha uharibifu wa mali,kuchoma moto magari , kuvunja milango na viio vya
baadhi ya maduka na kupora mali,ambapo watru kadhaa walijeruhiwa na wengine
kufariki kwa kupigwa risasi za moto.
Comments