CAF YATAJA WAAMUZI WA AFCON 2013 AFRIKA KUSINI
JOHANNESBURG, Afrika Kusini
SHIRIKISHO la Soka barani
Afrika (CAF) limetangaza waamuzi 18 na washika vibendera 21 kuchezesha mechi za
michuano ya Mataifa Afrika 2013, wakiwamo wawili raia wa Afrika Kusini, ambao
ni Daniel Bennett na Zakhele Siwela.
Mabadiliko mawili ya waamuzi
wapya na wasaidizi wao yamefanyika kwa kuongeza waamuzi wapya katika kundi la
waliochezesha fainali zilizopita za AFCON zuilizopigwa katika mataifa mawili ya
Equatorial Guinea na Gabon mwaka jana.
Orodha hiyo ya Caf inajumuisha
waamuzi wawili waliochezesha mechi mbili za fainali zilizopita, ambao ni Komlan
Coulibaly wa Malia (2010 - Angola) na Msenegali Badara Diatta (pichani kulia) wa fainali ya
mwaka jana kati ya Zambia na Ivory Coast jijini Libreville.
Coulibaly, 42, anatarajia
kuweka rekodi wakati atakapokuwa akicjhezesha fainali hizo za Afrika Kusini
zinazotarajia kuanza Januari 19. Hii itakuwa michuano yake ya saba tangu
alipoitwa kuchezesha katika fainali zake za kwanza mwaka 2002.
Waamuzi wawili wapya miongoni
mwa waliotajwa wametokea nchi za Kenya – Sylvester Kirwa, na Bernard Camille wa
Shelisheli, huku nchi za Algeria na Senegal zikitoa waamuzi wengi zaidi –
watatu kila moja.
Mohamed Benouza wa Algeria
hizi zitakuwa fainali zake za tano za Mataifa Afrika, kama ilivyo pia kwa Diatta,
aliyetajwa kuchezeasha fainali zote tangu alipoitwa kwa mara ya kwanza mwaka 2006.
AFCON 2013, zitakuwa fainali
za tatu kwa Bennett na za pili kwa Siwela waamuzi wa taifa taifa mwenyeji,
ambao watakuwamo pia katika fainali zijazo za Kombe la Dunia hapo mwakani
nchini Brazil.
Comments