Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Alliance for Democratic Change (ADC), Wilson Elias Mulumbe (katikati) aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Shoka Khamis Juma (kushoto) katika tukio lililofanyika Agosti 14, 2025 Njedengwa jijini Dodoma. Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kuchukua fomu, Mgombea pendekezwa wa Urais wa chama hicho, Mulumbe amesema kuwa chama chake kikishinda atahakikisha anafuta madeni yote wanayodaiwa wanafunzi na Bodi ya Mikopo, itakuwa elimu bure, afya bure na wateja wataunganishiwa umeme bure. Vyama vingine vilivyochukua fumu jana Agosti 13, 2025 ni; Chama cha Democratic Party (DP), Abdul Juma Mluya (Urais) aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Masoud Abrahman Khatib na Cha...
Comments