SERIKALI YAPATA MWEKEZAJI WA KUENDELEZA SEKTA YA KOROSHO HAPA NCHINI



Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika,  Mhandisi 
Christopher Chiza
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika,  Mhandisi 
Christopher Chiza (kushoto), akizungumza katika 
mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, 
kuhusu kupatikana  kwa mwekezaji raia ya Uingereza 
ambaye ameonesha nia ya  uendelezaji wa Sekta ya 
Korosho hapa nchini. Kulia ni Ofisa Habari Mkuu 
wa Wizara hiyo Richard Kasuga. (Picha habari na www.mwaibale.blogspot.com)


Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika,  Mhandisi 
Christopher Chiza (kushoto),akiongoza mkutano huo. 
Kulia ni mdau wa zao la korosho.
Wadau wa sekta ya korosho wakiwa kwenye 
mkutano huo
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika,  Mhandisi 
Christopher Chiza. (kushoto), akiongoza mkutano 
wa   uendelezaji wa sekta 
ya korosho.wengine ni wadau wa zao hilo.
Wadau wa kilimo wakiwa katika mkutano wa uendelezaji 
wa sekta ya korosho.

Na Dotto Mwaibale

SERIKALI imesema imempta mwekezaji kutoka nchini Uingereza ambaye ameonesha nia ya kuja kuwekeza katika sekta ya korosho hapa nchini.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Waziri wa Kilimo  Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza alisema mwekezaji huyo yupo nchini kwa ajili ya kukamilisha  mchakato huo.

"Kuna mwekezaji ambaye yupo nchini akikamilisha mchakato wa kuendeleza sekta ya korosho na tayari tumefanya naye mazungumzo kwa awamu mbili" alisema Chiza.

Alisema mwekezaji huyo anaangalia namna ya kujenga viwanda vya kubangua korosho na kusindika na kuwa lengo lake ni kuwainua wakulima kupitia  zao hilo na yeye mwenyewe kupata faida.

Chiza alisema Wizara ya Kilimo na Chakula wamekwisha fanya mazungumzo na mwekezaji huyo na juzi walikuwa naye wakikamilisha mchakati huo kwa kuwahusisha wakuu wa mikoa minne ya Pwani na Ruvuma pamoja na wadau wa zao hilo.

Alisema mwekezaji huyo anazungumza na wamiliki wa viwanda mbalimbali vya korosho ili kuona ni jinsi gani atafanya nao kazi.

Chiza alisema kwa muda mrefu kumekuwa na changamoto katika uuzaji wa zao hilo kupitia vyama vya ushirika ambapo ulisababisha tani  65 za zao hilo kushindwa kuuzwa na kubaki kwenye maghala.

"Viongozi wa vyama vya ushirika ambao hawakuwa waaminifu ndio waliosababisha kutokea kwa changamoto hiyo baada ya kukopa fedha katika mabenki na kushindwa kununua zao hilo'' alisema Chiza.

Alisema hapa nchini kuna viwanda vya kubangua korosho 12 vinavyo milikiwa na wazawa lakini kinachoendelea na kazi ni kimoja tu hivyo serikali imejipanga kuvikopesha ili viweze 

kufanya kazi na kupunguza changamoto ya korosho kuuzwa kwa bei ya chini.

Aliongeza kuwa pamoja na kuvifufua viwanda hivyo wanampango wa kubadilisha sheria ya korosho ya mwaka 2003 ili wapate mpya ambayo itakuwa na meno zaidi ya kuwabana walanguzi wa zao hilo.

Chiza hakuwa tayari kutaja jina la mwekezaji huyo kwa madai ni mapema kibiashara kwani wanaweza kuibuka watu wengine na kuharibu mchakato huo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO YANAYOUA NDOA NA MAHUSIANO

RAIS SAMIA ANA KWA ANA NA ZUHURA YUNUS

KANUNI 10 ZA MAHUSIANO YENYE FURAHA

HAKI 13 ZA MWANAMKE LAZIMA MWANAUME AZIHESHIMU:

JINSI YA KUMSAHAU EX WAKO ALIEKUACHA;

RAIS DKT.MWINYI: ZANZIBAR KUWA KITUO CHA BIASHARA CHA KIMATAIFA

USHAURI WA BURE KWA KILA MFANYAKAZI

ACHENI KUWA CHANZO CHA CHOKOCHOKO NA VURUGU - ASKOFU CHANDE