NAPE AWAPA UKWELI VIJANA


 Vijana Mmemsikia Kaka Nape Nnauye?         
                          Ujumbe wa Nape Nnauye - Mbunge wa Jimbo la Mtama kwa vijana wanataka nini Tanzania amewataka Vijana kutojaribu kuitoa serikali madarakani kwani kufanya au kujaribu kufanya hivyo ni kosa kubwa kisheria ikiwemo kushtakiwa kwa uhaini.

Akizungumza na Clouds fm Nape amesema ‘Ushauri wangu kwa vijana uzoefu na historia inaonesha duniani Kote mahali ambako zimetokea vurugu za kisiasa, waliochochea, waliohamasisha na walioanzisha sio waathirika wakubwa, Wao na watoto wao wako salama ila waathirika wakubwa ni wale walioenda kufanya’ Nape Nnauye

‘Wito wangu kama kaka mkubwa vijana wasihamasike kwenda kufanya ambalo hawajui matokeo yake, kubwa kuliko yote namna yoyote ya kujaribu kuitoa serikali iliyoko madarani,hata kumtoa rais aliyeoko madarakani kinyume cha katiba ni uhaini,ujue watu wanafanya kama masihala na adhabu yake ni kubwa sana,tusimung’unye maneno na nchini kwetu kosa la uhaini adhabu yake ni kubwa sana ni kifo’ Amesema nape.

Aidha amesema kuwa ni muda wa kusubiri tume iliyoundwa na Rais ifanye uchunguzi na itoe majibu nini kilitokea na maada ya hapo tujadili lakini kwa sasa Tusikurupuke.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MAPACHA WATATU FAMILIA YA MWAIKENDA WAPATA KIPAIMARA

𝐌𝐉𝐔𝐄 𝐊𝐀𝐂𝐇𝐄𝐑𝐎 𝐌𝐙𝐄𝐍𝐀

NAMNA YA KUTENGENEZA MAISHA YAKO KIMYA KIMYA

Wasifu wa Kizza Besigye

HAKUNA DHEHEBU LA DINI AMBALO LIKO JUU YA LINGINE, MADHEHEBU YOTE YAKO SAWA KISHERIA - RAIS SAMIA

MADAKTARI WALIPAMBANA KWA NGUVU ZOTE KUMNUSURU JENISTA MHAGAMA IKASHINDAKANA- MCHENGERWA

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️