"Hakuna Dhehebu Ambalo liko Juu ya Dhehebu lingine, Madhehebu Yote yako sawa Kisheria" ๐Kauli hii imekuja wakati ambapo
TEC imekuwa ikitoa matamko yenye Mwelekeo wa kukosoa au kutoa tahadhari juu ya mwenendo wa kisiasa, kiuchumi, au kijamii.
Serikali inapitia kipindi cha mjadala mkubwa kuhusu uhuru wa maoni, siasa za ushindani, na mahusiano kati ya serikali na taasisi za dini. Kumekuwepo maneno ya mgawanyiko mitandaoni kuhusu utendaji wa serikali ya awamu ya sita.
Rais anajibu mijadala hii kwa kujaribu kurejesha mjadala katika misingi ya utulivu, umoja ambayo imekuwa kaulimbiu yake mara kwa mara.
Tutazame Ujumbe kwa taasisi za dini๐
Rais Samia ameeleza wazi kuwa Matamko ya TEC yamekuwa mengi na yenye mgawanyiko ndani yao Anasema ndani ya Kanisa lenyewe kuna wanaopingana kuhusu matamko hayo.
Hii inaashiria kwamba serikali inaona baadhi ya matamko hayo hayawakilishi wote, hivyo kupunguza uzito wake wa kisiasa.
Anatoa onyo dhidi ya kutumia dini kama chombo cha mgogoro Hili ni jambo nyeti sana katika nchi yoyote.
Ametaja wazi kwamba “hakuna eneo baya la kumpata mtu kama dini”, akimaanisha nguvu ya dini inaweza kuwa chanzo cha kugawa jamii na kuanzisha migogoro ya hatari.
Anataka taasisi za dini zizingatie nafasi yao ya kufanya maadili, amani na mshikamano, badala ya kuingia kwenye malumbano ya kisiasa.
๐Ujumbe kwa wananchi na wapinzani Rais ametumia hoja kadhaa za msingi๐
Utawala wa demokrasia “Kama humpendi Samia, tustahimili tu... Ataongoza ataondoka.”
Serikali yake haipaswi kuangaliwa kama ya kudumu, bali kama inayofuata utaratibu wa kidemokrasia, hivyo hakuna sababu ya vurugu.
๐Kukosoa kunaruhusiwa lakini si vurugu Amesema watu wana haki ya kukosoa “kama amefanya makosa, semeni makosa yake.”
Huu ni ujumbe kwamba ukosoaji si tatizo, tatizo ni ukosoaji unaopelekea kuchochea mgawanyiko au vurugu. Kutotumia chuki ya kikabila, kidini au kibinafsi
Rais Aligusia suala la kumchukia kiongozi
๐Kwa asili yake
๐Kwa dini yake
๐Kwa alikotoka
๐Au kwa sababu za mitazamo binafsi
Hii inalenga kuzuia siasa za chuki ambazo Afrika zimeleta migogoro mikubwa.
Ujumbe kuhusu mafanikio ya serikali Rais ametaja “makosa” kwa mtindo wa balagha
๐Kuongeza huduma bora za afya
๐Kuboresha elimu hadi vijijini
๐Kukuza uchumi
๐Kuimarisha usalama
Serikali yake inaonekana kukosolewa kwa mambo ambayo kwake ni mafanikio, hivyo ukosoaji huo umejengwa kwenye hisia, si hoja.
Nihitimishe Uchambuzi huu kwa kusema
๐
Ujumbe huu una uzito kwa sababu Unalenga kuweka mstari kati ya dini na siasa, ili kuepusha mgawanyiko wa kijamii. Kukemea propaganda zinazolenga kuleta taharuki nchini.
Ni hotuba nzito kisiasa, kiusomi, na ki-uhusiano kati ya serikali na taasisi za dini, yenye lengo la kuongoza mjadala wa umma kuelekea utulivu na siasa za hoja, si chuki.
Mwenyezi Mungu Ibariki Tanzania, Mwenyezi Mungu Ibariki Africa na Viongozi wake Wote (Ameen)
Baki na Mimi kwa Mengi zaidi yanayo jiri Duniani
By Professor Chotara Mweusi Sultan kutoka viunga vya ๐
๐Sharif shamba
๐Ilala Dar es salaam
๐Tanzania
Bingwa la uchambuzi wa maswala ya kijamii, Uchumi na Siasa za Dunia Yetu.

Comments